simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mungu atupe nini Watanzania … kindonda?

with 2 comments

Hivi ni vionjo vichache sana katika mamilioni ya tunu ambazo Taifa letu limejaaliwa. Kwa nini wengine mnataka kuvuruga mazungumzo na majadiliano yanayohusu KATIBA yanayoendelea katika majukwaa mbalimbali hapa nchini. Wengi wameeleza kutoifahamu na hivyo kutoielewa Katiba tuliyo nayo sasa. Je, mazungumzo na majadiliano yanayoendelea si ndiyo msingi mzuri wa watu kujielewesha kuwa Katiba ni nini? Je, inasemaje? Je, inasaidia vipi katika kuendesha maisha ya siku hadi siku ya kila Mtanzania? Je, upungufu tunaouona katika maisha yetu … umaskini wa kipato … una uhusiano gani na kiwango cha ubora wa Katiba tuliyo nayo? Je, kuna chochote kinachoweza kufanyika ili kuongeza/kukuza ubora wa Katiba? Kama kipo, je, kuongezwa kwa ubora huo kutakuwa na mchango wowote katika kukuza vipato vyetu na hivi kuondokana na umaskini wa vipato? Je, tukiondokana na umaskini wa vipato, tutakuwa na maisha bora zaidi? Sote tuna wajibu wa kutoa elimu ‘sahihi’ kuhusu mazungumzo na majadiliano yanayoendelea.

KATIBA ndiyo SHERIA MAMA. Sheria zote zinatokana na katiba. Kwa hiyo, mantiki inaonyesha kwamba tukiwa na KATIBA iliyo na viwango vya juu vya ubora ndivyo tutakavyokuwa na sheria zilizo bora. Watanzania tuna tunu nyingi sana. Hebu tutulizane … tukomae … tuachane na ushabiki usio na msingi na tutunge SHERIA MAMA iliyo bora ili kujenga jamii iliyo imara, yenye dira, inayojua nini inataka, inasimamia misingi ipi, iwe na sauti yenye nguvu kiasi gani katika ulimwengu wa leo na ujao. Yote haya yanahitaji NIA ya dhati, SABABU ya dhati kwani UWEZO wa kuchukua mstari huo tunao. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu tubariki Watanzania, Mungu Ibariki Afrika.

Advertisements

Written by simbadeo

January 22, 2011 at 7:09 pm

Posted in Siasa na jamii

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. bw Simba nafurahishwa na kujifunza mambo mengi kupitia blog yako ombi langu kwako ni moja tu! mie ni mwalimu ninayewafundisha watz wenzangu ambao ni ndugu zako ila wananikatisha tamaa kwani hawajali shule na mahudhulio ni mabovu hebu email me tuchat pamoja unipe mbinu mpya nifanye kazi nzuri

  Like

  Mwalimu

  January 23, 2011 at 10:33 pm

 2. bw Simba nafurahishwa na kujifunza mambo mengi kupitia blog yako ombi langu kwako ni moja tu! mie ni mwalimu ninayewafundisha watz wenzangu ambao ni ndugu zako ila wananikatisha tamaa kwani hawajali shule na mahudhulio ni mabovu hebu email me tuchat pamoja unipe mbinu mpya nifanye kazi nzuri hapa Mwese sekondari.

  Like

  Mwalimu

  January 23, 2011 at 10:36 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: