simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

EWURA … mnashangaza

leave a comment »

EWURA yajitakasa bei ya gesi kupaa
na Tutindaga Mwakalonge

IMEELEZWA kuwa kupanda kwa bei ya nishati aina ya gesi nchini kumesababishwa na kuadimika kwa nishati hiyo katika soko la hapa ndani kwa takriban wiki mbili.

Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jana Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Uthibiti Nishati na Maji (EWURA) Michel Mshigwa alisema kuadimika kwa nishati hiyo kumesababishwa kuadimika kwake sokoni hivyo mitungi kuwa michache tofauti na matumizi.

Aidha, Mshigwa alielezea sababu nyingine kuwa ni uchache wa wateja na matumizi ya gesi hivyo inayoingizwa inawagharimu wafanyabiashara wakubwa katika usafirishaji na gharama nyingine pindi iingizwapo nchini.

Katika hilo aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika ununuzi wa gesi na matumizi yake kwa sababu kufanya hivyo kutapunguza gharama na itapatikana kwenye maeneo mengi zaidi.

“Matumizi ya gesi nchini yanapoongezeka ndivyo gharama ya gesi na kuadimika kwake kunapungua hivyo wananchi wasiogope kutumia gesi,” alisema.

Hata hivyo kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kunasababisha pia bei ya gesi kuwa juu kwa sababu uzalishaji wa nishati hiyo unategemea zaidi mafuta na kutumia fursa hiyo kuwaondoa wasiwasi watumiaji wa gesi kuwa bei ya nishati hiyo inaweza kushuka muda wowote kutegemea bei ya mafuta.

Kadhalika, ofisa huyo alibainisha kwamba serikali imeondoa kodi kwenye gesi hivyo EWURA haipati ruzuku kutokana na gesi na kitengo cha gesi huendeshwa kibiashara zaidi sababu inayowasukuma wafanyabiashara wa nishati hiyo kunategemea faida ipatikanayo baada ya mauzo.

Kwa sasa bei ya gesi imepanda kutoka sh 36,000 kwa mtungi wa kilo 15 kabla ya mwisho wa mwaka jana lakini kuanzia Desemba mwaka jana mtungi huo huuzwa kwa bei tofauti kati ya sh 55,000 na 70,000.

Chanzo cha habari: Tanzania Daima, 15 Januari 2011

Kichekesho. Bei ya mafuta ilipopanda soko la dunia … mafuta hayakuadimika katika vituo vya kuuzia mafuta. Kwa vile EWURA hawapati mgao wowote kutokana na mauzo ya gesi, basi wala hawaitazami, wala hawajali bei ipande isipande kwao sawa. TaaNeSco wanapotaka kupandisha bei ya umeme – hiyo kwao ruksa – maana na wao ile asilimia yao inakuwa NENE zaidi. Bei ya mafuta ikipanda – hiyo nayo ni sawa tu. Jamani EWURA hebu jisikilizeni wenyewe na kisha mtueleze ni kwa kiwango gani mmekuwa kichekesho na mnavyozidi kuwa mzigo kwa mtumiaji wa kawaida. Kazi ambayo kwayo Mamlaka yenu iliundwa … hamuitekelezi ipasavyo … kunani huko? Sasa mnavyotushauri kuwa watu wengi zaidi tununue na kutumia gesi … mnafikiri watu hatujui hilo … mnafikiri watu hatupendi kutumia gesi … mnafikiri watu tunapenda saaaaana kutumia mkaa na kuni na kupoteza muda kibao kuwasha na kupika …. Mjue tu kwamba mnaposhindwa kudhibiti bei ya gesi isipande ovyo … mnawasukumia kwenye matumizi ya kuni na mkaa hata wale wachache ambao tayari walikuwa wamekwisha ingia kwenye matumizi ya gesi … tunaelewa sana sula la ‘economies of scale’ … AU gei INAADIMISHWA kwa makusudi mazima ili kupata kisingizio cha kupandisha bei? Na tangu lini katika Tanzania hii BEI zikashuka … zikishang’ang’ania juu ni juu hata kama huko kwenye soko la dunia gesi itauzwa kwa shilingi 100 … sisi huku madhari bei ishafika huko ilipofika … itabaki hukohuko …. Jamani tusigeuzane watoto …! Kwa uchungu …

Advertisements

Written by simbadeo

January 16, 2011 at 1:26 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: