simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Shivji, Ulimwengu … Katiba Mpya

leave a comment »

Jenerali Ulimwengu … picha kutoka maktaba yangu

Shivji, Ulimwengu kuwasha moto wa Katiba Dar

na Nasra Abdallah

KONGAMANO kubwa kuhusu mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya linatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Januari 15, mwaka huu.

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), litawashirikisha wadau mbalimbali wakiwamo wananchi wa kawaida, makatibu kutoka vyama mbalimbali vya siasa, wasomi na viongozi wa asasi za kiraia.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti na Mratibu wa Makongamano wa Udasa, Dk. Kitila Mkumbo, alisema mada kuu katika kongamano hilo ni haja, maudhui na mchakato wa Katiba mpya.

Alitaja sababu hasa ya kongamano hilo na kusema kuwa wanalifanya pia kutokana na wadau wengi wa demokrasia na maendeleo kutoa wito wa kuandikwa upya kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Hata hivyo alisema kumekuwa na kusigana juu ya mchakato unaofaa kufuatwa katika kufikia Katiba mpya na kuongeza kuwa wananchi wengi wamekuwa wakihoji nini hasa matatizo ya Katiba iliyopo na maadhui gani yawekwe katika Katiba hiyo mpya.

“Hivyo basi lengo kuu la kongamano hili ni kutoa fursa kwa wananchi kuelewa misingi mikuu ya Katiba ya sasa na kutafakari kwa kina haja, maudhui na mchakato wa kupata Katiba mpya.

“Katika kufikia lengo hili, tumewaomba na wamekubali wananchi wawili waliobobea na wenye uzoefu wa muda wa kupigania demokrasia ili wawe wazungumzaji wakuu.

“Wananchi hao ni Profesa Issa Shivji, Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Julius Nyerere cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Jenerali Ulimwengu wa gazeti la Raia Mwema,” alisema mratibu huyo.

Kwa mujibu wa Dk. Mkumbo, wote hao wanafanana kwa jambo moja kwamba wametumia zaidi ya nusu ya maisha yao katika kupigania haki za wanyonge Tanzania na katika Bara la Afrika kupitia maandishi, machapisho na mihadahara inayoibua hisia, matumaini na wakati mwingine hasira.

Alisema pia kuwa watu hao ni miongoni mwa Watanzania wachache wanaoelewa historia ya mapambano ya kidemokrasia na ya kijamii ya Watanzania na Bara la Afrika kwa ujumla.

Alisema kwamba ni matarajio yao kuwa kongamano hilo litatoa mwongozo kuhusu maudhui na mchakato mwafaka katika kufikia Katiba mpya yenye kubeba matakwa na utashi wa Watanzania.

Pia alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Katiba na Sheria, ni miongoni mwa waalikwa katika kongamano hilo, ambapo aliwaomba wananachi bila kujali elimu zao kujitokeza kwa wingi.

Naye Mwenyekiti wa Udasa, Dk. Mushumbuzi Kibogoya, alisema kongamano hilo ni mwendelezo wa makongamano mengine, na kwamba mwaka huu utakuwa ni wa makongamano ya Katiba.

Dk. Kibogoya alisema kwa kuwa suala la uundwaji wa Katiba mpya linahitaji umakini ni vyema wananchi wakashirikishwa kwa karibu, kwani bila hivyo Katiba mpya inaweza kuja kuwa mbovu kuliko iliyopo sasa.

Alitoa tahadhari kwamba kufanyika kwa kongamano hilo si kuandika Katiba bali ni msingi wa kuandika Katiba, ambapo wananchi wataweza kuelezwa ni mapungufu gani yaliyoko kwenye Katiba ya sasa na kuweza kuchangia yale wanayoona yaongezwe kwenye Katiba au kuondolewa.

Chanzo cha habari: Tanzania Daima, 13 Januari 2011

Advertisements

Written by simbadeo

January 13, 2011 at 11:01 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: