simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mama Terezya Luoga …

leave a comment »

Mama Terezya Luoga, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais mwenye dhamana ya Mazingira alipokuwa mjini Kigoma hivi karibuni. Picha ni kutoka http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/waziri-luoga-atua-kigoma

Bei ya gesi imepanda tena … ndani ya kipindi kisichozidi miezi miwili tangu ilipopanda mara ya mwisho

Bei ya mtungi wa ujazo huu (Kg 15) yapata miezi mmoja na nusu iliyopita ilikuwa kati ya sh. 40,000 na 42,000. Hivi sasa bei imepanda hadi kufikia sh. 46,000.

Haya bei ya kuni … kuna mzigo wa sh. 2,000 na wa sh. 1,000 … uwezo wako tu …

Hivi karibuni Waziri wa Nchi, Terezya Luoga, alizungumza kwa hisia kali sana kuhusu uharibifu wa mazingira unaoendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi. Ni ukweli usiopingika kwamba shughuli za binadamu zimechangia kwa kasi kubwa sana katika kusababisha mabadiliko ya Tabia ya Nchi kiasi cha hata kuathiri misimu ya mvua. Tunaona kuongezeka kwa joto na vilevile ukame. Nchi yetu inategemea sana mvua kwa shughuli za kilimo.

Tukumbuke pia kwamba zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania (wanaozalisha) wamejiajiri katika kilimo (zaidi cha jembe la mkono). Papo hapo kadiri idadi ya watu inavyokua, ndivyo mahitaji ya nishati yanavyoongezeka.

Ulimwengu hivi sasa unasisitiza umuhimu wa kutumia nishati mbadala ambazo hazichangii sana katika uharibifu wa mazingira. Moja ya nishati hizo ni gesi ya asilia. Hivi sasa kuna idadi – japo si kubwa sana – ya Watanzania wanaotumia gesi kwa matumizi ya majumbani mwao. Lakini bei ya gesi imekosa utulivu kabisa. Jambo hili linaweza kusababisha hata kundi hili la watumia gesi kurudi kaitka matumizi ya mkaa na kuni. Hiyo ina maana kwamba miti mingi zaidi itakatwa. Hiyo inamaanisha uharibifu zaidi wa mazingira. Maana yake pia ni kwamba kilimo kitazidi kuathirika. Uzalishaji utapungua.

Pengine nimshauri Mama Terezya, ukali/hisia zake ni muhimu … lakini atumie mamlaka aliyo nayo kufuatilia kwamba kuna nini huko katika biashara ya gesi … mbona bei zake zinapanda kwa kasi kubwa hivyo … tena karibukaribu? EWURA wako wapi? Je, wao ni kukagua tu pampu za mafuta na kukubaliana na TANESCO kuongeza bei ya umeme? Kwa nini tuna chombo hiki kama bei zinapanda kiholela namna hii?

Advertisements

Written by simbadeo

January 10, 2011 at 6:33 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: