simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Vipi … nani awajibike?

leave a comment »

Kipande cha Barabara ya Nyerere katika eneo la Mtava hujaa maji sana nyakati za masika kama inavyoonekana katika picha hiyo niliyopiga mwezi wa 4 mwaka jana. Maji hayo huwa kero kubwa sana kwa watumiaji wote wa barabara kiasi cha kusababisha baadhi ya magari kuzimika au kukwama hapo.

Katika masika hayo ya mwaka jana … ililazimu kuchukua hatua ya dharura ili kuondoa maji hayo kwa haraka … hivyo mfereji ulichimbwa na kukatisha barabara hii ya pembezoni (service road) ili kuyamimina maji upande wa pili … hasa baada ya juhudi za kikosi cha kuzima moto kuyanyonya maji hayo kuwa za polepole mno …

Sasa ni miezi 8 imepita tangu uchimbaji huo wa mfereji ufanyike … lakini hakuna hatua zozote zilizofanyika ili kujengea vizuri mfereji huo (kwa kujengea makalvati) au hata kujenga upya kipande hicho cha barabara ili kufanya barabara hiyo iendelee kutumika. Hivi sasa barabara hiyo haitumiki kwa sababu tu ya mfereji huu. Je, mamlaka iliyotoa amri ya kuchimbwa kwa mfereji huu ni ipi … iko wapi … ina mpango gani na mfereji huu unaoifanya barabara hii ya pembezoni isiweze kutumika? Je, kwa nini uzembe kama huu usitafsiriwe kwamba ni kuhujumu uchumi wa nchi …? Huu si ndiyo ufisadi katika sura nyingine? Jamani, wajibikeni katika maeneo yenu!

Advertisements

Written by simbadeo

January 9, 2011 at 1:53 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: