simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Katiba Mpya … ukombozi wa mnyonge?

leave a comment »

Jana, Alhamis 30 Desemba 2010, nilifuatilia sehemu ya kipindi cha majadiliano kilichorushwa na ITV. Majadiliano yalikuwa juu ya ‘Ongezeko la bei ya umeme’. Nilivutiwa na mambo mengi sana yaliyozungumzwa pale. Nilipata picha pia EWURA pamoja na kuwa ni chombo kilichoundwa kwa sheria ya Bunge bado haina nguvu ya kuhimili kile ambacho pengine wanasiasa wanakitaka (kwa kutoa misukumo yao wakiwa nyuma ya pazia). Reveletions nyingine zilikuwa za kushtua.

Mathalani: Bw Mlaki alitoa takwimu kwamba mwaka 2005, TANESCO ilitumia kiasi cha asilimia 49 ya mapato yake yote ya mwaka mzima ili kulipa kampuni zinazoiuzia umeme. Mwaka uliofuata TANESCO ililipa asilimia 104 ya mapato yake yote kwa kulipia gharama hizo. Kwa takwimu hizo tu peke yake mtu unaona kwamba TANESCO ni kichekesho cha karne – si ajabu wakaingizwa hata kwenye Guiness Book of Records.

Kingine ni takwimu kwamba viongozi wa ngazi za juu serikalini hupewa ‘bure’ units kati ya 1200 hadi 1440 za umeme kwa mwezi. Nisingekuwa na ugomvi na jambo hilo endapo tungekuwa tukijitosheleza kwa asilimia 100 kwenye bajeti yetu. Lakini hadi sasa tunajitosheleza kwa asilimia 60 tu. Hizo asilimia 40 ni misaada na mikopo kutoka nje. Sasa kwa mantiki hiyo … hiyo anasa ya kupeana units hizo bure kabisa inatoka wapi? Hivi sasa hatuna budi kuhakikisha tunafunga mikanda (namkumbuka Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Cleopa Msuya miaka ile ya themanini alipokuwa Waziri wa Fedha aliwahi kusema kwamba kila mmoja abebe msalaba wake na tukubali kufunga mikanda – watu walinung’unika sana – lakini alikuwa sahihi mno na nadhani somo alilotoa bado halijatuingia akilini). Ndiyo, tunachohitaji ni kuondokana na kuweka mbele starehe ili tuweze kujitegemea na kuondokana na utegemezi unaotuumiza (kama huo wa TANESCO).

Sasa basi, hili la TANESCO ni ‘just a tip of an iceberg’ … kuna madudu mengine mengi zaidi serikalini na katika jamii. Tunahitaji kufanya ‘overhaul’ ya mfumo mzima ili tuanze kwa namna iliyo madhubuti. Na mahali pa kuanzia ni KATIBA MPYA. Kwani kuna tatizo gani kama tutaandika katiba mpya sasa … maana nilimsikia Mh. Jaji Werema, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akisema ‘kuandika katiba mpya kwa sasa hapana’ … sijui anataka ije iandikwe lini wakati hapa tulipofikia maji si ya shingo tena bali tumezama na tuyabugia kwa kasi? Ukombozi wa kweli utatokana na kuandikwa Katiba Mpya … na jambo hili ni la haraka kuliko mambo mengine yote. Ndiyo ninavyoona mimi.

Advertisements

Written by simbadeo

December 31, 2010 at 10:39 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: