simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Kigoda … ni dawa

leave a comment »

Vigoda mbalimbali katika duka la bidhaa za sanaa za mikono linalokwenda kwa jina la MIKONO, karibu na Chang’ombe VETA. Kwa maelezo ya Mzee mmoja, rafiki yangu, mtu ukijizoeza kutumia viti aina ya vigoda … hutapatwa na matatizo ya mgongo. Siku hizi watu wa umri kuanzia miaka 35 na kuendelea hulalamika sana kuhusu maumivu ya mgongo. Pengine ni wakati sasa turudi kutumia bidhaa/vitu vyetu vya asili. Hoja ya mzee wangu huyu ni kwamba viti vya siku hizi … hasa vile vya kunesanesa na kujizungusha … vinalemaza uti wa mgongo kwa kasi sana. Alikazia hoja yake kwa maelezo kwamba hata madaktari siku hizi, wanashauri sana watu walale kwenye vitu vigumu … hata godoro linatakiwa lile ambalo halitafanya uti wako wa mgongo ujipinde … wengine wanakwenda mbali zaidi na kusema kuwa si vibaya kulala chali sakafuni kwa muda fulani. Kwamba mambo haya ni kweli au si kweli … nakuachia wewe msomaji kuamua kulingana na uzoefu wako. Ciao!

Advertisements

Written by simbadeo

December 30, 2010 at 6:11 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: