simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Uchakachuaji … kansa inayoenea kila sekta ya jamii

leave a comment »

Picha hizo hapo juu ni za embe zinazofahamika kwa jina maarufu la ‘za kupepea’.

Seti hii ya picha 2 zinazofuatia ni za embe zilizo maarufu kwa jina la ‘mdondo’.

Tafakari ya leo:

Kuna tofauti kubwa sana kati ya embe za kupepea na zile za mdondo. Embe za kupepea ni zile zilizofikia ukubwa fulani katika mchakato wa kukomaa. Lakini kabla hazijakomaa kabisa na kuiva … wafanyabiashara (wakishirikiana na wakulima) huzitungua embe hizo na kisha kuzilazimisha kukomaa (kwa njia ya kuzipepea ili ziive kwa moshi na joto la moto) na kisha kuziingiza sokoni. Kwa mtindo huu, embe iliyopepewa inawahishwa sokoni takribani wiki mbili kabla ya muda ambao ingeutumia kwa njia ya kimaumbile (natural). Ubora wa embe za kundi hili huwa ni wa mashaka. Mara nyingi ukila moja hutatamani kuongeza nyingine kwa sababu ni chachu/kali kupita kiasi.

Embe za kundi la pili, yaani, zinazoitwa mdondo, hizi ni zile ambazo hukomaa mtini na hata kuivia mtini mpaka kufikia hatua ya kuanguka yenyewe. Embe hizi hufuata utaratibu wake wa kiasili/kimaumbile hata kuwa kwake tayari kuingizwa sokoni. Embe hizi huwa na ubora zaidi kulinganisha na hizo za kundi la kwanza. Hizi ni tamu … tamu sana. Ukila moja si ajabu kuongeza ya pili, na ya tatu … kama una ubavu.

Miaka ya nyuma ilikuwa aghalabu kukutana na embe za kupepea, lakini siku hizi hali imebadilika sana … inakuwa vigumu zaidi kukutana na embe ‘mdondo’. Sababu yake kuu ni kuwa wafanyabiashara (na wakulima) wana shauku kubwa sana ya kuanza biashara kiasi cha kukosa subira ya maumbile kufanya kazi yake.

Kwa kutumia mfano huu wa embe, tunaona mambo mengi yanayofanana na hayo katika jamii yetu, nitatoa mifano michache:

1. Katika elimu – kuna kipindi tulipata walimu waliopewa jina la ‘Voda fasta’; tuna shule nyingi tu (zinazoitwa za Kata) ambazo nyingi zinaendeshwa/zinasimamiwa/zinahudumiwa na walimu wasiozidi watano (imagine – hawa wanapaswa kufundisha kuanzia kidato cha 1 hadi cha 4!); nimewahi kuzungumza na wahadhiri wa vyuo vikuu – wengi wanalalamikia ‘aina ya wanafunzi wanaojiunga huko’ kwamba siyo ‘university material’ – kisa – mambo ya tuisheni za mitaani zinazofundisha mtu kupasi mitihani hata kama hapati stadi zilizokusudiwa. Kuna mengi mengine katika elimu.

2. Katika afya – changamoto za ‘uchakachuaji’ ni nyingi – na hasa katika ubora wa viwango vya watoa huduma. Kuna malalamiko mengi kutoka kwa wahudumiwa na hata kutoka kwa watoa huduma wa muda mrefu kwamba watoa huduma wengi ‘hawajui kazi’.

3. Katika uongozi – nilisoma swali la Ndg Nape Nnauye (DC wa Masasi) kupitia Facebook akihoji namna maandalizi ya viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM yasivyokidhi viwango … ni haraka haraka tu ili kupata uongozi … hata kama kukomaa kwa mambo bado.

Kuna mambo mengi katika sekta za kijamii yanayoweza kulinganishwa na kile tunachoweza kujifunza kutokana na embe ‘za kupepea’ na zile za ‘mdondo’. Tuendelee kutafakari ili kuona tunajikwamua vipi na hali hii katika jamii yetu kwa manufaa ya Taifa letu la leo na kesho. Mungu tubariki.

Advertisements

Written by simbadeo

December 29, 2010 at 12:21 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: