simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Boxing Day … haikupita vivi hivi

with one comment

Kwa wengine Boxing Day iliishia vibaya … Ni ajali niliyoikuta maeneo ya Malamba Mawili katika barabara inayounganisha Mbezi Louis na Kinyerezi. Ajali ilihusisha gari aina ya saloon yenye namba za usajili T 312 AVB dhidi ya jamii ya VRS yenye namba za usajili T 331 AWD. Ajali ilitokea kwenye moja ya kona nyingi za barabara hiyo. Kwa maelezo ya mashuhuda, dereva wa saloon alibana sana upande usio wake ili kupata kona vizuri, wakati huohuo dereva wa VRS alikuwa akija kutoka upande wa pili kwa mwendo mkali na ndipo ilipotokea ajali hiyo. Zaidi ya mshtuko na michubuko hapa na pale abiria na madereva waliokuwa kwenye magari hayo walitoka salama. Mpaka kamera hii inaondoka eneo la ajali … askari wa usalama wa barabarani walikuwa bado hawajawasili hapo. Madereva … ni vema kuzingatia mwendo kasi wa wastani hata katika barabara zisizo na magari mengi. Tunaweza kupunguza ajali na hivyo kuokoa uhai wa watu pamoja na mali zinazohusika.

Advertisements

Written by simbadeo

December 26, 2010 at 10:25 pm

Posted in Siasa na jamii

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. Nawapa pole sana kwa wote ambao boxing day kwao ilikuwa huzuni badala ya furaha.

    Like

    dorine

    December 28, 2010 at 3:27 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: