simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Uhuru … niwatakie heri

leave a comment »

Kutoka katika nyumba alimowahi kuishi Hayati Mwalimu J.K. Nyerere pale Pugu Sekondari

Muasisi wa Taifa la Tanzania, Hayati Julius K. Nyerere

Tanzania (au tunaweza kusema Tanganyika) inaadhimisha miaka 49 tangu ipate uhuru wake kutoka kwa wakoloni (Waingereza). Ni kipindi kirefu. Ni karibu kabisa ya nusu karne. Ni karibu sawa na umri wa kuishi wa Watanzania (siku za nyuma ilikuwa miaka 42, sasa hivi wastani umepanda zaidi kidogo). Kama nchi bado tunakabiliana na changamoto nyingi. Safari bado ni ndefu na majaribu ni mengi.

Baadhi ya changamoto tunazokabiliana nazo kama Taifa ni pamoja na:

1. Matatizo makubwa ya maji kwa matumizi ya majumbani, viwandani, maofisini, kwenye taasisi mbalimbali na mashambani (kwa kilimo cha umwagiliaji)
2. Kuna matatizo makubwa kuhusiana na ajira – zaidi ya asilimia 90 ya watu wanaozalisha mali (zinazoonekana na zisizoonekana) wako katika ajira zisizo za uhakika wa kipato – nyingine ni za kutia fedheha. Kuna changamoto nyingi katika kuleta fursa za ajira za uhakika na zenye kipato chenye heshima.
3. Huduma za afya – bado ni kitendawili kikubwa. Upatikanaji wa dawa katika zahanati na hospitali umeshuka sana.
4. Elimu imebaki ya kubabaisha – kuna shule nyingi zaidi ndiyo – lakini ubora wa elimu inayopatikana katika shule hizo ni wa kuhuzunisha.
5. Miundo mbinu bado ni finyu na mara nyingi ni mibovu.
6. Orodha ni ndefu.

Tufanye nini

1. Tuimarishe mshikamano na utaifa
2. Tuwe tayari kujitoa sadaka (kufunga mikanda) kwa ajili ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo – kukuza ubunifu, kuongeza uzalishaji mali, kukazania kubadili mifumo yetu ya uchumi kutoka kutegemea wahisani na kilimo kwenda katika uzalishaji wa viwandani
3. Kujielemisha kwa bidii ili kwamba maarifa tunayopata popote pale ulimwenguni na katika vitabu na vyanzo vingine vyovyote tuyalete nyumbani na kuyafanyia kazi kila mmoja wetu kwa nafasi yake
4. Tubane matumizi – yale yasiyo ya lazima (yaani ya anasa) tuyaache kwa ajili ya vizazi vyetu vitakavyoishi Tanzania hii miaka 200 ijayo na kuendelea
5. Kuna mengine mengi ambayo wewe msomaji unayafahamu.

Tuende wapi

1. Tunataka tuwe Taifa linalojitegemea kikamilifu na lenye uchumi na demokrasia imara katika dunia nzima (siyo lazima tuwe a super power)
2. Tunataka tuwe Taifa la watu wenye afya njema (kimwili, kiakili na kiroho)
3. Tunataka tuwe Taifa lenye msimamo madhubuti katika kuhusiana kwake na mataifa ya nje
4. Tunataka tuwe Taifa linalosaidia mataifa mengine na binadamu wa mataifa hayo ili kufanya Dunia iwe mahali bora zaidi pa kuishi

Tunaweza ikiwa mimi na wewe na yule tutatimiza wajibu wetu kwa uaminifu na kwa ukamilifu

Watanzania wenzangu popote pale mlipo ninawatakia heri na baraka tele kwa sikukuu hii kubwa kabisa katika Taifa letu. Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika, Mungu Tubariki Watanzania.

Advertisements

Written by simbadeo

December 8, 2010 at 5:06 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: