simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mbezi Msigani … maji

leave a comment »

Mbezi Msigani ni kitongoji kipya katika jiji la Dar es Salaam. Ni kitongoji kipya kwa sababu idadi ya wakazi katika eneo hilo imeongezeka katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Eneo hili tayari lina huduma mbalimbali … umeme na barabara kuu moja iliyo katika kiwango cha changarawe/moramu.
Kilio kikubwa cha wakazi wa eneo hili ni maji. Maji yamekuwa bidhaa adimu kupita kiasi. Umbali kutoka Mbezi Mwisho mpaka eneo hili hauzidi kilometa 2 – hata hivyo DAWASCO bado hawajawafikishia wakazi wa eneo hilo maji.
Tayari kuna miundo mbinu ya maji inayofahamika kwa jina maarufu kama ‘Mabomba ya Wachina’, lakini tangu miundo mbinu hiyo ijengwe … tayari miaka miwili imepita na hakuna hata tone moja la maji limewahi kufikishwa huko kwa miundo mbinu hiyo.
Je, huduma za maji ya kusambazwa na malori zinagharimu vipi? Niliuliza. Ilibidi niombe kigoda nikae maana nilichoshwa na jibu nililopata.
“Tanki la lita 1000 tunauziwa kwa shilingi 10,000,” alinijibu mwenyeji wangu. Lo, hebu fikiria familia yenye watu sita (ambao ni wastani wa familia nyingi hapa jijini Dar es Salaam), matumizi yao ya maji kwa siku, kwa wiki, kwa mwezi yakoje. Je, mtu mwenye kipato cha wastani wa shilingi 200,000/= kwa mwezi atamudu vipi huduma hiyo ya maji?
“Sisi tuna wasiwasi na watu wa DAWASCO … hawa ndiyo wenye miradi hii ya malori yanayosambaza maji huku … ndiyo maana hawataki kufanya juhudi za sisi kupata huduma ya maji kupitia mradi wa mabomba ya Wachina … si bure … kuna jambo!” ananiambia mwenyeji wangu. Haya, kazi kwa Mbunge mpya wa Ubungo … kazi kwa Waziri (si mpya) wa Maji.

Advertisements

Written by simbadeo

December 5, 2010 at 12:27 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: