simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Vitabu – maonesho Ubungo Plaza

leave a comment »

Unapoingia unakutana na bango hili …

Mandhari katika ukumbi wa maonesho …

Kujisomea …

Tukubali tu kwamba watoto wanapenda kujisomea … matatizo yapo kwetu wazazi … hatununui vitabu … hatusomi vitabu … unakataa?

Wajasiriamali wengine hawakukosekana … tunawapongeza kwa kutumia fursa hiyo kuwaunga mkono wachapishaji vitabu.

Pongezi nyingi ziwafikie TANAPA – Tanzania National Parks – kwa kuwaunga mkono wachapishaji kwa ushiriki wao. Naamini uwepo wao katika maonesho haya ya vitabu umesaidia katika kutia chachu na kuvuta watu wengi zaidi kuyatembelea. Mwendeleze utamaduni huo.

Wakati siku ya leo wanaapishwa mawaziri walioteuliwa na Mh Rais kusimamia wizara mbalimbali, wachapishaji vitabu (ambao kwa kweli tasnia yao imeyumba sana) wana matumaini makubwa kwamba waziri mpya wa elimu na mafunzo ya ufundi, Mh Shukuru Kawambwa, atatoa kipaumbele kwa vitabu na tasnia nzima ili kukuza viwango vya usomaji na biashara ya vitabu kwa ujumla. Kwa sasa hivi tukubaliane kwamba hali inatisha … Picha chache zilizo hapo juu zinasema mengi …

Mosi: Wachapishaji wanajitahidi kuchapisha vitabu pamoja na kwamba hali ya biashara ya vitabu ni ngumu;

Pili: Wasomaji wa vitabu na watu wanaoonesha hamu ya kusoma vitabu ni watoto … lakini wao siyo wanaotoa fedha kununua vitabu … matokeo yake … watoto hawapati vitabu … ni wazazi wachache sana wananunulia watoto wao vitabu … mara nyingi ni mpaka wapigiwe kelele na walimu … kwa hiyo huishia kununua vitabu vya mosomo peke yake … vitabu vya kujisomea kwa burudani na kukuza maarifa havipewi nafasi … havina mtetezi.

Tatu: Serikali haina budi kufanya juhudi za makusudi kukazania ukuzaji wa viwango vya usomaji vitabu nchini. Ikiwepo nia ya dhati ya kisiasa … tutaona mabadiliko ya kweli.

Nne: Waandishi na wachapishaji … endeleeni kufanya kazi yenu kwa ufanisi pasipo kukata tamaa. Mambo yatajipa tu one day!

Advertisements

Written by simbadeo

November 27, 2010 at 6:37 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: