simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Vitabu … maonesho yanaanza leo Ubungo Plaza

with 2 comments

Wiki ya Maonesho ya Vitabu Tanzania inaanza leo katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Barabara ya Morogoro, Dar es Salaam. Vitabu ni hazina ya maarifa na stadi. Kwa kusoma vitabu tunakuza uwezo wetu wa kufikiri, kubuni, kutunga, kukabili changamoto za kiakili, vilevile tunaburudika na kuelimishwa;hata kujikosoa kunaweza kupatikana kutokana na usomaji vitabu. Gazeti la leo la Daily News linaripoti kwamba Viwango vya Usomaji nchini Tanzania vimeporomoka sana kwa zaidi ya asilimia 30 ukilinganisha na miaka ya 70. Kumbe basi, sisi sote kila mmoja wetu ana wajibu na jukumu la kuona namna gani anakuwa sehemu inayosaidia kukua kwa viwango vya usomaji. Nunua kitabu – japo kimoja kwa mwezi – wananunulie watoto vitabu – vile vya shule lakini pia vile vya kujisomea. Bila shaka tutaanza kuona MABADILIKO chanya katika jamii yetu – kimtazamo, katika kuzama kwenye fikra, kiuchambuzi wa mambo (na hiyo itatusaidia kuondokana na hali ya kubebwa mzobemzobe katika utoaji wa uamuzi kuhusu masuala yanayotuhusu sisi pamoja na maisha yetu ya sasa na ya baadaye).

Pichani ni moja ya duka maarufu la vitabu katika jiji la Dar es Salaam: The Dar es Salaam Printers Limited. Hili lipo Mtaa wa Jamhuri maeneo ya Posta, Dar es Salaam. Litembelee ufurahie vitabu vilivyo pale.

Advertisements

Written by simbadeo

November 25, 2010 at 11:17 am

Posted in Siasa na jamii

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. ni vizuri kuadhimisha siku ya vitabu kama hivi huku tukijiuliza ama tukijadili ni kwanini waandishi wa vitabu wamefanywa kuwa watumwa wa wachapishaji. mwaandishi atumapo mswada kwa mchapishaji kama utakubaliwa kitabu chake kitachapishwa huku mwandishi ama mtunzi akilipwa mrahaba wa asilimia kumi.ina maana kama kitabu kitauzwa hadi milioni 100 mwandishi atalipwa milioni 10.
  bila shaka huu ni utumwa tena mbaya sana ni hali inayokatisha waandishi tamaa kabisa watu wanaofanya kazi wanabaki kuwa watumwa wa watu wasiofanya kazi.ovyo ovyo!

  Like

  mandela pallangyo

  February 24, 2014 at 12:29 pm

  • Ndugu Pallangyo

   Una hoja nzito. Ni muhimu wachapishaji wapitie upya mikataba yao na waandishi/watunzi wa vitabu. Hii ni hasa pale idadi ya nakala inazidi, tuseme nakala elfu 20,000. Chini ya hapo, asilimia 10 ni sawa.

   Pamoja sana.

   Like

   simbadeo

   February 28, 2014 at 8:40 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: