simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Makongoro Mahanga …

with 6 comments

… alivyopokelewa katika Jimbo la Segerea.

Nilikuwa katika pitapita zangu. Nilishangaa kuona foleni ndeefu ya magari. Naelewa kwamba si jambo la ajabu sana katika barabara hii ya Tabata-Segerea … lakini kulikuwa na utofauti fulani. Mbele kidogo ndiyo nakutana na msafara wa pikipiki, waenda kwa miguu … na magari… wengi katika msafara huo wakiwa katika fulana na kofia za CCM. Ndipo bango lililokuwa limebebwa mbele likanitaarifu kwamba ni msafara wa Mbunge wa Segerea aliyechaguliwa hivi karibuni, Mh. Makongoro Mahanga.

Well, kama ilivyo kawaida mtu unabaki na maswali mbalimbali:

1. Hivi ndivyo wabunge wote (au karibu wote) walivyopokelewa majimboni mwao?
2. Je, shamrashamra hizi zinaashiria ‘kumalizika kwa kazi’ au ‘kuanza kwa kazi’?
3. Mbona vijana ndiyo walitawala … ni kizazi kipya?

Kwa maoni yangu … sasa tuweke kampeni pembeni na kuanza kazi. Watu wetu hawana ajira, watu wetu wanaishi katika makazi duni, elimu wanayopata watoto wetu ni duni, huduma mahospitalini zinahitaji kazi ya ziada ili kupandisha viwango vyake vya ubora, usalama wa raia, miundombinu, upatikanaji wa huduma za maji safi na salama, upatikanaji wa huduma nzuri za kuzoa taka ngumu na taka kimiminika, well … kuna mambo mengi sana yanayotuhitaji.

Wakati huohuo tukumbuke kwamba kuna kesi imefunguliwa mahakamani na aliyekuwa mgombea katika jimbo hilo, Bw. Freddy Mpendazoe, akilalamikia matokeo ya kura zilizopigwa tarehe 31 Oktoba 2010 … naamini Watanzania wengi wana hamu ya kujua nini itakuwa hatma ya kesi hiyo. Haya, hilo ni la Mahakama na tuwaachie wao wafanye kazi yao.

Kwetu sisi wananchi … tunachohitaji ni kuwekewa mazingira ya kuweza kukuza uzalishaji, kuongeza tija na hivyo kukuza vipato vyetu ili tuweze kumudu kujiletea maendeleo katika nyanja zote muhimu: afya, elimu, makazi, usafiri, mawasiliano, nishati n.k.

Tuendelee kuwepo!

Advertisements

Written by simbadeo

November 21, 2010 at 11:20 am

Posted in Siasa na jamii

6 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. nahiyaji vifaranga 500 naweza kupata ?

  Like

  mikdady juma

  June 11, 2015 at 3:44 am

 2. nahitaji vifaranga 500 naweza kupata ?

  Like

  mikdady juma

  June 11, 2015 at 3:45 am

  • Habar mick ninauza vifaranga wa kienyej kwa gharama nafuu sana nipo dar kimara tuwasilianebkwa no. 0754078015

   Like

   gimase

   December 9, 2015 at 12:25 pm

 3. Pata incubator kwa gharama na fuu sana Pata full automatic incubator ya mayai 54KwawshshLaki 8.5
  zikiwa na ufanisi wa 89nangarantiiiyaymwakakmmojajaTupo dar kimara. Pia tunauza vifaranga wa kienyeji. 0754078015.

  Like

  Gimase

  December 9, 2015 at 12:35 pm

 4. Keep these arceilts coming as they’ve opened many new doors for me.

  Like

  Tommy

  May 9, 2017 at 8:04 pm

 5. kemarin hubungi panitianya udah habis ya tempatnya… Rian Say : komputer tersedia buat blogshopnya cuma 40 bang, itu udah penuh. kalo bawa laptop sendiri masih bisa kok bang. dateng aja

  Like

  high risk auto

  May 20, 2017 at 9:02 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: