simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Uchaguzi … hali ilivyokuwa vituoni

leave a comment »

a href=”https://simbadeo.wordpress.com/?attachment_id=2001″ rel=”attachment wp-att-2001″>

Niligongana na wanahabari wa CAPITAL TELEVISION pale Segerea Magereza polling station … wanachapa kazi

Kituo cha uchaguzi katikati ya barabara – ni katika barabara inayounganisha Tabata Dampo na Kigogo … du tumekosa hata maeneo mengine ya wazi?

Mtaa wa Kongo … ulipwaya … hasa upande wa Kituo cha Polisi Msimbazi

Katika Mtaa wa Sikukuu na Aggrey … kweupeee

Mtaa wa Kongo unapokutana na Aggrey … kumepwaya isivyo kawaida …

Kwa Ofisa Mtendaji Kata … maeneo ya Bungoni Ilala …

Buguruni … Shule ya Msingi Hekima … makarani wakipumzika … maana hakuna wapiga kura wengi ati …

Buguruni Chama … vituo kibao … wapiga kura ‘wengine wameingia mitini’ …

<

Buguruni kwa Mnyamani … shwari … japo palipwaya …

Mitaa ya Vingunguti karibu na Kituo Kidogo cha Polisi huko Vingunguti …

Pamoja na uchaguzi mkuu kuwa wa shwari katika maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam, bado kuna dosari ndogondogo kadhaa zilizojirudia. Baadhi ya dosari hizo ni pamoja na:

1. Baadhi ya wapiga kura kutoona majina yao
2. Baadhi ya wapiga kura kuwa na vitambulisho lakini namba za vitambulisho na zile zilizo kwenye daftari kutofautiana
3. Ulegevu wa baadhi ya makarani wa TUME … kwani wengine hawakuwa wepesi kueleleza wapiga kura nini wafanye pindi wanapokutwa kwamba wana dosari fulani … sasa sijui mafunzo hayakukolea au labda usingizi ulikuwa ukiwasumbua … maana wengine walilala vituoni ili kuhakikisha ratiba inakwenda vema

Kutokana na namba 3 hapo juu, ninashawishika kufikiri kwamba baadhi ya wapiga kura waligeuka na kuondoka zao hasa kwa sababu hawakujua wamwone nani ili kuwatatulia matatizo yao … wapo waliohofia kwamba wanaweza kuonekana kuwa ni watukutu na hivyo kuishia mikononi mwa sheria … kwa hiyo hatua nyepesi kwao ni kuondoka badala ya kuuliza vema zaidi … hili sasa ni la elimu ya uraia.

Matokeo yanaendelea kutoka … mpaka sasa kwa mujibu wa vyombo vya habari … vyama vya upinzani vinajitahidi katika kupata viti vya ubunge na vya udiwani … wanapata zaidi kuliko ilivyokuwa 2005 … tuendeleze amani … sote tunaweza kuwa washiriki wazuri kati

Advertisements

Written by simbadeo

November 1, 2010 at 3:46 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: