simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Majongoo … ubunifu

with one comment

Nimewahi kusikia mara nyingi ikisemwa kwamba hakuna jipya chini ya jua. Tazama mtindo huo wa usukaji nywele. Unaitwa ‘Majongoo’. Wengi wetu tunawafahamu viumbe wanaoitwa hivyo. Watu wa umri wa mtoto – humpenda sana jongoo – husisimua akili na fikra mbalimbali za ulimwengu wao. Na kuna imani nyingi zimejengeka kuhusu jongoo. Utasikia watu wakiambizana: Usitutupe kama unavyomtupa jongoo na mti wake. Basi, wabunifu walimtazama mdudu/kiumbe huyo na kuibuka na mtindo huo wa nywele. Hivi sasa uko kwenye chati. Ni akina mama wengi tu – hasa wa mijini – wanaosuka mtindo huo. Tuenzi ubunifu. Tusome vema mazingira yetu kwani humo ndimo tunamotoa ubunifu wa mambo mbalimbali.

Maumbile hutupa mafunzo mengi sana. Wazee wetu walikuwa na desturi ya kulima kipande fulani cha ardhi kwa miaka mitatu minne mpaka mitano, kisha hukiacha kwa miaka mingine mitatu, minne au zaidi. Sababu yake ilikuwa kuhakikisha kwamba ardhi haichoki. Siku hizi kipande cha ardhi kitalimwa mwaka nenda mwaka rudi … kikichoka … tunawekea mbolea ya viwandani … matokeo yake aina ya mazao yanayotoka hapo yanabeba kemikali ambazo huishia miilini mwetu … kwa nini kansa na maradhi mengine ya aina hiyo yasiwepo kwa wingi? Tujifunze kutoka kwenye maumbile. Unapofika wakati wa kupumzisha kitu, acha kipumzike ili baadaye kije kuwa na manufaa kwako tena … tena kwa kiwango cha juu, au siyo?

Advertisements

Written by simbadeo

October 25, 2010 at 3:15 pm

Posted in Siasa na jamii

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. Naihitaji kusuka majongoo nisaidie nimpate msusi mzuri

    Like

    Upendo

    November 30, 2017 at 10:28 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: