simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Alfu Lela U Lela … umesoma?

with 6 comments

Baadhi ya vitabu katika mfululizo wa hadithi maarufu sana ulimwenguni kote – Alfu Lela U Lela au Siku Elfu Moja na Moja na kwa kimombo ni The Arabian Nights.

Kushoto ni mimi. Kulia ni mfasiri wa mfululizo ulio kamilifu zaidi wa hadithi za Alfu Lela U Lela, Mzee Hassan Adam. Yeye vilevile ni mtoto (wa kambo) wa mwandishi na mshairi mashuhuri kupita wote katika Afrika ya Mashariki, Hayati Shaaban Robert. Mzee Hassan amefasiri upya mfululizo wa hadithi hizo zisizokwisha utamu kutoka katika maandiko ya Kiingereza, Kijerumani na Kiarabu. Anazimudu vema lugha zote hizo tatu. Kwa miaka mingi amekuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Cologne huko Ujerumani. Ama kwa hakika ana mengi ya kutufundisha. Kama hujasoma hadithi hizi au ungependa kuzisoma ili kupata uhondo wake kikamilifu basi hii ni fursa yako. Niandikie nikufahamishe utapata vipi vitabu hivyo ambavyo kwa kweli ukianza kuvisoma hutaviweka chini. Kama wewe ni mwandishi wa hadithi … kwa kusoma vitabu hivyo utajitafakari ni namna gani ukuze zaidi kipawa chako cha uandishi ili nawe hadithi zako ziwe na mashiko kwa mamia ya miaka. Usikose.

Advertisements

Written by simbadeo

October 18, 2010 at 11:22 pm

Posted in Siasa na jamii

6 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. nahitaji kupata nakala za vitabu hivyo. maana ni long time sana hadi nimeanza kusahau kama vina exist. Tafadhari sana nifahamishe wapi kwa kuvipata

  Like

  Godfrey Elias

  July 16, 2011 at 1:42 pm

  • Ndugu Godfrey, vitabu hivyo vinapatikana katika bookshops jijini Dar es Salaam. Unaweza pia kupiga simu 022-2865411 kwa ajili ya kuvinunua. Kila la kheri na nakutakia usomaji mwema.

   Like

   simbadeo

   July 16, 2011 at 8:12 pm

 2. Habari za kazi kaka?mimi nahitaji hivi vitabu vya alfu lela u lela, ni bookshop ipi vinapatikana?

  Like

  Taji

  May 6, 2013 at 1:47 am

  • Hi Taji

   Habari zako? Nadhani utembelee Tanzania Publishing House, Mtaa wa Samora, karibu na Mnara wa Bismin (Askari) … bila shaka utavipata … lakini waweza kujaribu kwenye bookshop yoyote kubwa hapa Dar.

   Like

   simbadeo

   May 7, 2013 at 11:11 pm

 3. Ni vitabu vizuri kwa kweli

  Like

  SELINA S. NICEAS

  March 28, 2014 at 11:05 am

 4. Mm naviitaji vitabu hivyo lakini niko nnje ya nchi kwasasa nipo Qatar ntavipataje?

  Like

  bakari juma

  January 10, 2016 at 2:34 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: