simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Slaa: Niko tayari kula mihogo Ikulu …

leave a comment »

Ni kauli aliyoitoa mgombea Urais kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt Wilbrod Slaa, katika moja ya mikutano yake ya kempeni. Alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba hatakuwa tayari kula mapochopocho wakati wananchi wana njaa.

Ni kauli nzito. Ni ahadi nzito. Macho ya Watanzania pamoja na masikio yao yataelekezwa kwake endapo atafaulu kuingia Ikulu na ikiwa kweli ataishi kauli hiyo. Kwa uzoefu, mahali pengi duniani wagombea hutoa ahadi za kujinyima … lakini mara waingiapo … husahau ahadi zao. Miongoni mwa marais ambao wamefaulu sana kuishi kile walichokiahidi … kuishi maisha yasiyotofautiana sana na ya raia wao ni pamoja na Juan Evo Morales wa Bolivia, Lula da Silva wa Brazil, Mahmoud Ahmadinejad wa Iran (pamoja na migogoro aliyo nayo na mataifa ya Magharibi), Mzee Nelson Mandela (enzi za uongozi wake) vilevile Paul Kagame wa Rwanda. Hawa ni marais katika zama zetu ambao waliishi/wanaishi maisha ‘simple’ na kwa kiasi kikubwa wamefanya mambo makubwa mazuri katika mataifa yao.

Sisi wengine kula mihogo na machungwa ishakuwa kawaida. Uchumi hauruhusu kupata chamchana kwa kiasi kisichopungua shilingi 2,000. Lakini kipande cha muhogo cha shilingi 500 na maji ya shilingi 200 au chungwa la shilingi 200 – hivyo tunamudu. Tunaishi maisha ya kufunga mkanda, kujibana ili tuufikie mwisho wa mwezi mwingine. Baada ya hapo basi ni michapo na kusoma magazeti chini ya kivuli cha mti. Ukirudi ofisini unakuwa na nguvu mpya. Unachapa kazi kwa kwenda mbele. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika. Mungu tubariki na sisi.

Advertisements

Written by simbadeo

October 16, 2010 at 1:07 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: