simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Kariakoo … Bomoabomoa

with one comment

Kamera ya Waza Mpaka Basi ilidaka tukio hili la kuvunjwa kwa majengo yaliyo kwenye kona ya Mtaa wa Tandamti na Nyamwezi pale Kariakoo, Dar es Salaam leo. Bila shaka majengo haya yanavunjwa ili kupisha ujenzi wa ‘pengine’ jengo jipya na la kisasa … mimi naona ni yaleyale ya siku zote … tunabomoa si majengo tu bali hata historia yetu … Dar es Salaam ina nafasi kibao, kwa nini majengo hayo mapya ‘ya kisasa’ yasijengwe huko? Kwa nini tusipanue jiji hili kwa majengo mapya, makubwa, ya kisasa, yanayozingatia upangaji miji huko pembezoni?

Haya, katika bomoabomoa hiyo, wapo waliojipatia riziki … wenye uwezo wa kung’oa nondo, madirisha … kila mmoja alikuwa anajichukulia chake … Bongo! Kichekesho.

Askari wa Jiji (Manispaa ya Ilala) nao hawakucheza mbali … lakini wao attention yao kubwa ilikuwa kwa wafanyabiashara ndogondogo … tazama huyo wanavyomdakua … mali anazouza … karoti na nyanya na bilinganya … thamani yake haizidi shilingi elfu tano (TZS 5,000). Hivi, hakuna kazi ya maana zaidi wanayoweza kufanya askari hawa? Je, mshahara wanaolipwa ni kwa ajili ya kukamata bidhaa za wafanya biashara ndogondogo? Hivi hizo karoti na bilinganya wakazikamata … zinakwenda wapi? Je, askari hawa wanachangia vipi katika uchumi na ukuaji wa jiji la Dar es Salaam? Au ndiyo tumekosa ubunifu wa kuwatumia hawa kwa namna yenye tija zaidi kwao na kwa jiji letu na kwa taifa kwa ujumla?

Advertisements

Written by simbadeo

October 9, 2010 at 5:11 pm

Posted in Siasa na jamii

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. Tanzania ina wanasiasa na haina viongozi kwa sasa. kama wanabomoa majengo ya kihistoria ujue kwamba vichwani mwao kumejaa upupu na elimu feki.

    Nadhani dawa ni sisi wananchi kuzinduka na kuwakaanga live ili wajue kwamba nchi siyo mali yao hii.

    Like

    gano

    October 10, 2010 at 8:21 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: