simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Quality plaza … motoni

leave a comment »

Quality Plaza kwa nje leo asubuhi

Eneo lililoungua

Ultimate Security … walishiriki kuzima moto huo jana usiku

Moja ya corridor nzuri katika jengo la Quality Plaza … pamoja na uzuri huo kuna kitu kinakosekana … fire extinguishers … je … vipi ofisi zilizo kwenye jengo hili? Zina fire extinguishers?

Baadhi ya wafanyakazi wa Quality Group, ambayo ina ofisi zake kwenye jengo la Quality Plaza na ambao moja ya ofisi zao ndiyo iliyoathirika, wakiwa nje kusubiri utaratibu kutoka kwa wakubwa wao.

Jengo la Quality Plaza ni moja ya majengo muhimu katika jiji la Dar es Salaam. Kuna ofisi nyingi muhimu kama vile mabenki (benki tatu), ofisi za kampuni ya ndege, mgahawa, wachapishaji vitabu, hivi karibuni pia imeongezeka ofisi inayoratibu utoaji wa leseni mpya za udereva n.k. Katika kipindi kisichozidi miaka miwili kumekuwa na matukio matatu ya moto … ikiwa ni pamoja na hili la jana. Bila shaka umefika wakati sasa, kampuni inayosimamia uendeshaji wa jengo hili, Image Properties, waite wataalamu na kufanyia tathmini mfumo wa umeme na mifumo ya huduma nyingine ili kuona kama bado viko katika viwango vinavyostahili. Vinginevyo majanga ya moto na mengineyo yataendelea kuathiri jengo hili na wapangaji wake … tusisubiri mpaka maisha ya watu yapotee ndipo tuchukue hatua. Wakati ni huu … matukio yaliyokwishatokea ni dalili za kutosha.

Advertisements

Written by simbadeo

September 24, 2010 at 10:15 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: