simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

CHADEMA … uzinduzi ulivyokuwa … jicho la pembeni

with 3 comments

Wapo waliovaa fulana zenye ujumbe kama huo na zaidi …

Wapo waliojigeuza akina ‘Zakayo’ ili wapate kuona vema na wasipitwe na kitu …

Nyomi. Mwenyekiti, Mbowe: wengi wenu mmekuja kwa miguu au magari yenu … siku ile watu WALIBEBWA … kutoka Morogoro, Chalinze, Bagamoyo …

Mwenyekiti: Hatutamwaga damu hata ya Mtanzania mmoja ili Slaa aingie Ikulu … lakini tutasimamia haki yetu

Biashara ilinoga …

Kuelekea jukwaa kuu. Slaa: Ndani ya siku 100 za kwanza tutafanya mengi makubwa … serikali ndogo … katiba mpya … muundo mpya wa serikali … ajira za maana … lengo ni kuigeuza Tanzania iwe nchi yenye kutegemea uchumi wa viwanda … kuifanya Tanzania isiwepo tu miongoni mwa mataifa bali iwe nchi yenye sauti inayosikilizwa … wawekezaji wasiwe wale wa kuja kukwapua na kuondoka bali wawe wale wa kuja kuwekeza hapa na mali INABAKI hapa … Marekani wana watu milioni 400, wana mawaziri wasiozidi 14, Tanzania ina watu milioni 40 … ina mawaziri 47 … wakati wa MATUMAINI MAPYA … uchaguzi huu ni uchaguzi wa UKOMBOZI …

Ujasiriamali kazini …

Umma: Sema usiogope sema … Ndiyo walivyokuwa wakiimba.

Nilichoona:
1. Kulikuwa na usikivu mkubwa … ni watu wachache sana waliokuwa wakipitapita huku na huko
2. Akina mama hawakuwepo kwa wingi … bado najiuliza kwa nini?
3. Uhuru wa kuongea bado unapata kwikwi nyingi miongoni mwa watu … wanataka kusikia wengine wanavyojitoa mhanga kuongea hadharani.
4. Niliongeza msamiati jana: Wanasanii wanaharakati.

Advertisements

Written by simbadeo

August 29, 2010 at 3:41 pm

Posted in Siasa na jamii

3 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Watanzania angalia viongozi wasio na huruma wanavyo ihujumu Nchi na Mashirika yanayotusaidia.

  Ni chukizo kubwa kuona mtu mmoja anasababisha kusimamishwa kwa misada mikubwa kama hii. Je JK yupo? Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu Tanzania walipeleka malalamiko juu ya ubadhirifu wa Dr. PAUL SD.MUSHI kwa Rais Kikwete lakini kilichofanyika ni Rais Kurudishia Mwizi huu malalamiko ambayo kwayo aliitisha kikao na kuwatukana wafanyakazi.

  Angalieni sasa uozo huu na mwingine uliofichika TET

  UNIDO unhappy over Dar’s funds misuse
  Th e United Nations Industrial Development Organization, UNIDO, in Dar es Salaam is livid with officials of the Tanzania Institute of Education responsible, for among others, curriculum development for primary, secondary schools and teaching colleges.
  The source of the bad blood between the two institutions lie in the latter’s alleged misuse of funds extended by UNIDO for a study which would have enabled the Tanzania Education Institute to develop a new entrepreneurship curriculum for secondary schools.
  A meeting held on Friday, April 16th 2010 at the Institute’s headquarters at Mikocheni, on the outskirts of Dar es Salaam between top flight UNIDO and the Institute’s officials ended acrimoniously as the former demanded to know why the money they had provided to the institute had not been used for the intended project.
  Meanwhile UNIDO said further disbursement of funds to the Tanzania Education Institute had been suspended awaiting consultations with their bosses at the UN agency’s headquarters in Geneva, Switzerland.
  One of the issues which apparently angered UNIDO officials was the absence of the Institute’s Chief Executive Officer, Mr Paul Mushi who was reported to be outside the country on official trip.
  UNIDO officials could not understand how the CEO could leave the country without first ensuring that the money that had been extended to his institution by the UN agency had been judiciously used for the intended project.
  “We will find out from his bosses (the CEO’s superiors) who had allowed him to travel abroad without first finishing the work we had both agreed on,” the UNIDO officials said.
  Interestingly, senior Institute’s officials who attended the meeting with the UNIDO officials were completely in the dark over the provision of funds by the UN agency.
  They told UNIDO officials that they did not know that the UN agency had provided funds to their institute for the development of the entrepreneur curriculum for secondary schools.
  They said the only thing they were aware of was that their institute was supposed to have started planning how to develop a new entrepreneur curriculum for secondary schools.
  For a long time Mr Mushi has been repeatedly criticized for spending most of his time travelling outside the country instead of concentrating on his work.
  A few weeks ago, he is reported to have bumped in Sweden with his boss, the Minister for Education and Vocational Training, Professor, Jumanne Maghembe.
  Apparently, Professor Maghembe was supposed to have linked up with the Institute of Education’s IT man in Sweden where they were expected to have attended a crucial meeting during which the latter would have been expected to play a crucial role in the meeting.
  However, Mr Mushi is alleged to have usurped the trip which should have been used by his IT man. Professor Maghembe is reported to have been extremely furious, questioning Mr Mushi on why he had travelled to Sweden when the trip was not meant for him.
  “Where is the IT man from your institute? I don’t need you…I want your IT man…this trip was meant for him…” a source in the minister’s delegation quoted the Professor as saying.
  According to well informed sources at the Institute, Mr Mushi’s predecessor, Dr Naomi Katunzi had left behind a lot of money when she left the institute.
  However, Mr Mushi is alleged to have spent all the money in his endless foreign travels. Mr Mushi has continued with his go-happy trips at a time when his institute is supposed to be providing the nation with answers to the present falling education standards!
  Last year the institute lost 80 new computers which had just been bought when thieves broke at night into the strong-room where they had been stored.
  To date it is not however, known what steps were taken by the CEO in finding out who was behind the theft which had all the hallmarks of being an inside job.
  In the words of employees at the Tanzania Education Institute Mr Mushi’s leadership is currently under question. They have spoken on the need of getting the CEO out of the institute as soon as possible before the institute, currently reported to be in the red, collapses.

  UNIDO kutofurahishwa kwa matumizi mabaya ya ruzuku Dar
  Shirika la Umoja wa Mataifa lihusikalo na Kuendeleza Viwanda, UNIDO jijini Dar-es-Salaam limekasirishwa na watendaji wa Taasisi ya Elimu Tanzania, miongoni mwa mengi ikiwemo utengenezwaji wa mitaala kwa elimu ya msingi, sekondari na vyuo.

  Chanzo cha kuzuka kwa mkanganyiko kati ya taasisi hizo mbili unaibuka baada ya shutuma za hivi karibuni zilizotolewa na UNIDO kutokana na tafiti ambayo ingewezesha Taasisi ya Elimu Tanzania kutengeneza mtaala mpya wa elimu ya ujasiriamali kwa shule za sekondari.

  Katika kikao kilichofanyika mnamo ijumaa, 16 Aprili 2010 makao makuu ya taasisi hiyo, Mikocheni nje kidogo ya jiji la Dar-es-Salaam kati ya viongozi wa juu ya UNIDO na watendaji wa taasisi hiyo kiliisha kwa ukali baada ya kuomba kufahamu kwanini fedha zilizokuwa zimetolewa hazikutumika katika mradi uliokusudiwa.

  Kwa sasa shirika hilo la UNIDO limesema kutolewa tena kwa ruzuku kwa Taasisi ya Elimu Tanzania kumesitishwa ikisubiriwa majadiliano na mabosi wengine katika makao makuu ya shirika hilo la Umoja wa Mataifa jijini Geneva, Uswizi.

  Moja ya suala lililowakasirisha maofisa wa UNIDO ni kutokuwepo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Bwana Paul Mushi ambaye ameripotiwa kuwa nje ya nchi kwa safari ya kikazi.
  Maafisa wa UNIDO walishindwa kuelewa namna gani Mkurugenzi Mkuu anaondoka nchini bila ya kuhakikisha fedha zilizopewa taasisi yake toka kwa shirika la Umoja wa Mataifa zimetumika katika mradi uliokusudiwa.

  “Tutang’amua toka kwa mabosi wake (wakuu wa Mkurugenzi Mkuu) ambao walimruhusu kusafiri ng’ambo bila ya kumaliza kwanza kazi ambayo wote tulikubaliana” alisema afisa wa UNIDO.

  Chakushangaza zaidi, maafisa wa ngazi za juu wa taasisi hiyo waliohudhuria kikao na maafisa wa UNIDO hawakuwa na ufahamu kabisa juu ya kutolewa huko kwa ruzuku na shirika hilo la Umoja wa Mataifa.

  Waliwaambia maafisa wa UNIDO, hawakufahamu kuwa shirika la Umoja wa Mataifa lilitoa ruzuku kwenye taasisi yao kwa ajili ya kutengeneza mtaala wa elimu ya ujasiriamali kwa shule za sekondari.

  Walisema jambo ambalo wanalifahamu tu ni taasisi yao ilitakiwa kupanga namna gani wataanza kuandaa utengenezwaji wa mtaala mpya wa elimu ya ujasiriamali kwa shule za sekondari.
  Kwa muda mrefu sasa, Bwana Mushi amekuwa akikosolewa mara kwa mara kwa kutumia muda wake mwingi kusafiri nje ya nchi badala ya kumakinia kazi yake.

  Wiki chache zilizopita iliripotiwa alikutana na bosi wake, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Jumanne Maghembe huko Uswidi (Sweden).

  Kwa wakati huo, Profesa Maghembe alitakiwa kuunganishwa na mtaalamu wa mawasiliano na teknolojia wa Taasisi ya Elimu Tanzania nchini Uswidi (Sweden) ambapo walitarajiwa wangehudhuria kikao muhimu ambacho walitarajia angetoa mchango mkubwa katika kikao hicho.

  Licha ya hivyo, Bwana Mushi ameshutumiwa kunyang’anya safari ambayo ilikuwa mahsusi kwa mtaalamu wa mawasiliano na teknolojia.

  Profesa Maghembe aliripotiwa kukasirishwa sana, na kumhoji Bwana Mushi kwa nini alisafiri Uswidi (Sweden) wakati safari haikuwa imemlenga yeye.

  “Yupo wapi mtu wa mawasiliano na teknolojia toka katika taasisi yako? Sikuhitaji wewe….namtaka mtu wako wa mawasiliano na teknolojia…safari hii ilikuwa inamlenga yeye….” chanzo cha taarifa toka katika msafara wa waziri kilimnukuu Profesa.

  Kwa mujibu wa vyanzo vinavyoaminika katika taasisi hiyo, mtangulizi wa Bwana Mushi, Dk. Naomi Katunzi aliacha fedha nyingi kipindi akiondoka katika taasisi.

  Licha ya hivyo, Bwana Mushi ameshutumiwa kutumia fedha zote katika safari zake za nje zisizo isha. Bwana Mushi ameendelea na safari zake za fahari kipindi ambacho taasisi ilipaswa kutoa majibu kwa taifa juu ya kushuka kwa kiwango cha elimu!

  Mwaka jana, taasisi ilipoteza kompyuta themanini (80) ambazo zilikuwa zimenunuliwa muda mfupi kabla wezi hawajavunja chumba cha hazina na kuiba kompyuta ambazo zilikuwa zimehifadhiwa humo.

  Mpaka leo haijajulikana hatua zilizochukuliwa na Mkurugenzi Mkuu katika kutafuta kujua nani alihusika na wizi ambao kwa kiasi kikubwa unaonekana kuwa ni mpango wa ndani humo katika taasisi hiyo.

  Kwa maneno mengine mwajiriwa wa Taasisi ya Elimu Tanzania, Bwana Mushi hajatumikia ipasavyo.

  Wakiongelea hitaji la haraka la kumwondoa Mkurugenzi Mkuu katika taasisi hiyo mapema iwezekanavyo. Taasisi hiyo hivi sasa inaripotiwa kuwa katika hali mbaya ya kuporomoka.

  Like

  HUJUMA NZITO

  October 7, 2010 at 2:22 pm

 2. FAKE

  Like

  TIE

  December 11, 2010 at 2:55 pm

  • Ungefafanua kidogo … ingekuwa poa zaidi. Kumbuka, una haki ya kutoa maoni yako ili mradi huvunji sheria za nchi na kwingineko duniani, au siyo?

   Like

   simbadeo

   December 13, 2010 at 5:03 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: