simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Kilimo Kwanza …

leave a comment »

Wakati ambapo Tanzania imekumbatia sera inayotoa kipa umbele kwa shughuli za kilimo, wapo wajasiriamali ambao nao wameelekeza mitaji yao kwenye eneo hilo muhimu kwa uchumi wa nchi. Binafsi natoa pongezi nyingi sana kwa wadau hawa muhimu wa uchumi wa Taifa letu. Hata hivyo, pamoja na nia yao nzuri, ni vema tukumbuke kuwa wazalendo vilevile. Tunapofanya biashara tujitahidi sana kuleta bidhaa zenye ubora unaostahili. Matrekta na zana nyingine za kilimo ni nyenzo muhimu sana za kuimarisha shughuli za kilimo nchini. Kumbe basi tulete matrekta na zana hizo zinazokidhi viwango bora vya ubora. Nimefurahi kuona kwamba matrekta yanapatikana kwa urahisi zaidi hivi sasa nchini kulinganisha na miaka ya nyuma. Hivi sasa ni pesa yako tu. Unaingia show room na unatoka na trekta lako. Kikubwa kama nilivyosema hapo awali msituletee matrekta bomu, matrekta fake. Tunahitaji matrekta imara yatakayodumu na ambayo spea zake zinapatikana kwa urahisi na katika viwango ambavyo watu wetu watavimudu. Ujanja ujanja uwekwe kando.

Napongeza juhudi za watu binafsi kama hao wanaoendesha biashara hiyo hapo juu ya matrekta. Tunaamini kwamba matrekta hayo yanayouzwa hapo ni bora kwa viwango vinavyotarajiwa. Kilimo Kwanza inawezekana!

Advertisements

Written by simbadeo

July 23, 2010 at 6:53 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: