simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Uhuru … kweli?

leave a comment »

Ni picha ya mwezi Juni 2008. Ni katika makutano ya barabara ya Bibi Titi na ile ya Uhuru (Mnazi Mmoja). Kila ninapoitazama huwa ninaingia kwenye fikra nzito sana. Uhuru. Ni neno lenye fasiri nyingi sana. Kuna nchi kujipatia Uhuru wake kutoka kwa utawala wa nchi nyingine. Kuna kitu kinazungumzwa sana siku hizi, Uhuru wa kujieleza, Uhuru wa vyombo vya habari, Uhuru wa kuamua mtu ufanye nini. Uhuru. Uhuru.

Mwaka huu kwa utaratibu wa ‘demokrasia’ yetu tunafanya uchaguzi. Tutachagua Rais, Wabunge na Madiwani. Kila aliyejiandikisha ana uhuru wa kumchagua yule ambaye yeye anafikiri kwamba ataongoza vema zaidi katika nafasi anayogombea. Ili kutumia uhuru huu wa kupiga kura … ni muhimu sana vyama vya siasa, taasisi zisizo za serikali, taasisi za serikali, vyombo vya habari na watu binafsi kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha kwamba elimu ya uraia inatolewa kwa mapana na marefu ili kila mpiga kura kwanza kabisa ajitambue (apate kuwa na fikra huru) ili kufanya uchaguzi baada ya kufanya tafakari yakinifu (informed choice).

Ndugu yangu aliyeketi hapo kwenye picha bila shaka ni raia wa nchi hii, bila shaka ana sifa za msingi za kumwezesha kupiga kura. Ili atoke katika hali hiyo ya kuomba na kuanza kujipatia maisha kwa kufanya uzalishaji … anastahili kuwezeshwa kifikra na kisaikolojia ili ajitambue…atambue thamani yake kama binadamu na thamani yake katika kujiletea yeye mwenyewe pamoja na jamii yake mabadiliko yaliyo chanya.

Tunaweza kuleta mabadiliko hayo … lakini ni lazima kwanza kubadili mitazamo yetu … tuwe na mitazamo inayotupa uhuru zaidi kuliko kuufungia uhuru huo. Sote tunawajibika katika kusaidiana kupata mitazamo chanya kuhusu maisha na thamani zetu kama binadamu.

Advertisements

Written by simbadeo

July 15, 2010 at 10:03 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: