simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Maji na ujasiriamali …

with one comment

Nimekuta pikipiki hii ikitoa huduma ya usambazaji maji maeneo ya Kinyerezi Darajani. Ni ubunifu mzuri. Ni moja ya njia za kuwafikishia watu huduma ya maji karibu. Dereva wa pikipiki hiyo aliniambia kwamba mjasiriamali mwenye kampuni hiyo ya Dolphin Water sasa ina pikipiki zipatazo 500 zinazosambaza maji katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya Kinyerezi, Mongolandege, Banana, Sitakishari, Majumbasita, Ukonga Mwembe Madafu, Mombasa, Gongolamboto, Kipunguni, Kitunda n.k.

Napongeza wazo hili. Labda kilichonistua ni bei. Ndoo moja ya lita 20 wanaiuza kwa shilingi 200. Ni kiasi kikubwa. Naelewa kwamba kuna maeneo katika jiji la Dar es Salaam wananunua ndoo moja ya ujazo huo kwa zaidi ya kiasi hicho cha fedha. Lakini shilingi 200 kwa ndoo ni ghali sana, nafikiri ndoo moja ingeweza kabisa kuuzwa kwa shilingi 100 au chini ya hapo. Tukumbuke kwamba haifai kutumia matatizo ya watu katika jamii ili kujitengenezea ‘super profit’. Labda ni wakati sasa wajasiriamali wakaelewa hilo kwamba suala si kutengeneza faida kubwa tu, bali pia kuona kwamba hata watu wa kawaida wanafikiwa na huduma zao. Familia yenye watu sita hutumia wastani wa ndoo 10 kwa siku. Hiyo ina maana shilingi 2000. Kwa mwezi tunazungumzia shilingi 60,000. Kwa mtu anayepata mshahara wa shilingi 200,000 kwa mwezi, tayari bajeti ya maji peke yake inazidi asilimia 25. Naamini upembuzi yakifinifu ukifanyika kuhusu mtindo huu wa ufikishaji huduma za jamii kwa watu basi unaweza kufanywa kwa ufanisi zaidi na kwa gharama nafuu. Wajasiriamali, eneo lingine linalohitaji huduma za namna hii ni uzoaji taka. Jiji na halmashauri zake wameelemewa. Sekta binafsi iingilie kati na kutoa huduma hiyo hasa katika mitaa ya pembezoni.

Advertisements

Written by simbadeo

July 3, 2010 at 12:49 pm

Posted in Siasa na jamii

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. That is wonderfull, Very creative!

    Like

    Elieshi

    October 3, 2011 at 2:58 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: