simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Ajali Tabata Segerea …

leave a comment »

Ajali ni kati ya daladala lenye namba za usajili T736 ATN na gari dogo lenye namba za usajili T604 AEV. Daladala hilo linafanya safari zake kati ya Segerea na Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Mashuhuda hawakawii kujaa…

Unaweza kuona jinsi dereva wa daladala alivyobana upande usio wake na kuacha nafasi kuuuubwa kushoto kwake.

Baada ya kusababisha ajali, dereva wa daladala, ambaye jina lake halikutambulika mara moja, alitimua mbio. Wasamaria wema hawakumwacha afike mbali. Walikwenda kumuibua kule alikokuwa. Hapa wakimpa kichapo cha kishkaji.

Salama yake ilikuja alipojitoma kwenye gari dogo aliloligonga.

Dereva wa gari dogo, aliyefahamika kama Baba Pati, akiwa kwenye majonzi baada ya tukio hilo la gari lake kugongwa na daladala.

Nafasi iliyoachwa na dereva wa daladala ilikuwa kubwa kiasi cha kuruhusu hata malori madogomadogo kupita.

Foleni nayo haikukawia kujiunda … pande zote mbili za barabara.

Imetokea majira ya saa 4 hivi asubuhi ya leo katika moja ya kona kali za barabara ya Tabata kwenda Kinyerezi eneo la Tabata-Segerea. Uzembe wa mtu mmoja unaweza kuleta madhara makubwa sana. Hatuna budi kuwa na nidhamu tunapoendesha vyombo vya moto. Kikubwa ni kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa katika ajali hii ya leo. Ajali zinaepukika.

Advertisements

Written by simbadeo

July 3, 2010 at 1:12 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: