simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mazingira …

leave a comment »

Wiki mbili zilizopita nilichapisha picha za maeneo hayo mawili. Hivi sasa takataka zimeongezeka zaidi hapo. Kuna matrekta ya manispaa za jiji la Dar es Salaam yanayopita katika mitaa kusomba takataka. Swali ni kwamba zamu ya matrekta hayo kuja Barabara ya Nyerere kusomba takataka hizo ni lini?

Tela la moja ya matrekta ya Manispaa ya Kinondoni lililokwama Barabara ya Nyerere kwa zaidi ya siku tatu sasa. Tatizo linaloonekana bayana kwenye tela hilo ni pancha. Hivi kweli pancha tu inaliweka tela hilo kwa siku tatu na zaidi? We’ve got be serious guys!

Dr Batilda Buriani, waziri anayehusika na mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais. Wiki hii alipokuwa Bungeni alinukuliwa akisema: “…kila mmoja na awe askari wa kutunza mazingira … ukimwona mwenzako anatupa taka ovyo barabarani …mkemee…Kuna mikakati ya kulisaidia jiji la Dar es Salaam na majiji mengine …”.

Suala kubwa ni kujenga moyo wa kuwajibika kwa vitendo vyetu. Kama manispaa ya Moshi wameweza … kwa nini manispaa nyingine zishindwe … hasa za jiji la Dar es Salaam. Mbona ni mahodari sana wa kunyang’anya mali za machinga kuliko kusomba takataka hizi … na kodi kibao tunalipa?

Advertisements

Written by simbadeo

June 23, 2010 at 10:17 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: