simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Shirika la Elimu Kibaha …

leave a comment »

Shule ya Sekondari Kibaha – moja ya shule bora nchini.

Maktaba ya Umma – Kibaha

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Jamii (Ufundi) – Kibaha, Bw. Baradyana. Chuo hiki ni sehemu ya Shirika la Elimu Kibaha.

Tumbi Hospital. Ni sehemu ya Shirika la Elimu Kibaha.

Lengo la kuanzishwa kwa Shirika hili la Elimu Kibaha ilikuwa ni kutengeneza modeli ya taasisi zenye lengo la kutokomeza maadui wakubwa watatu wa nchi yetu ya Tanzania, yaani, umaskini (kupitia utoaji elimu ya ufundi inayowawezesha vijana kujiajiri na kujitegemea), maradhi (huduma za afya kupitia hospitali ya Tumbi) na ujinga (kupitia shule ya msingi ya Tumbi na Shule ya Sekondari ya Kibaha na nyinginezo zilizo hapo). Kulikuwa na bado zipo shughuli nyingine nyingi zinazoedeshwa chini ya Shirika hili.

Pengine ni wakati sasa Serikali yetu iendeleze nia ya kuanzishwa kwa Shirika hili – kwanza ianze na kuliimarisha shirika hili ambalo sasa baadhi ya miundo mbinu yake imeanza kuchoka. Pili, kila mkoa uanzishe Shirika la aina hii ili kuendeleza vita dhidi ya maadui wetu wakuu watatu, na sasa yupo adui wa nne – ufisadi – huyu naye hatuna budi kumpiga vita na kumshinda. Mikoa ipewe malengo ya kuwa imeanzisha taasisi za aina hii ndani ya kipindi cha miaka 10 ijayo. Inawezekana. Kupitia sera ya Kilimo Kwanza, taasisi kama hii inaweza kuleta aina ile ya mageuzi ya kimaendeleo tunayotaka kuleta nchini.

Advertisements

Written by simbadeo

June 20, 2010 at 11:38 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: