simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Archive for June 20th, 2010

Entrepreneur of the day …

leave a comment »


I’m sitting in my small office. In walks a young man carrying a bag. He shows me the products he is selling. I havent taken my lunch and it is well past 2pm. I’m attracted by his products. It is groundnuts, well packaged and the colour is also very attractive. The price is also reasonable for the amount of each packet. I decide to buy 2 packets that my children will love as part of gifts I send them from time to time.

The young man is none but Thomas Nyitati. He has formed a group of young people. They buy groundnuts from farmers. They grade them and prepare them nicely before packaging. Once packaged, they take them out to find buyers.

This is one example in which youths of the country could very much utilise their time and energy in ways that are paying both to them and their country. In so doing they will very much help build the economy of this developing country. Promoting locally produced products should be given a priority. We should support such young entrepreneurs. Hongera Thomas na wenzako.

Pictured above is Thomas and the products he sells. You can contact him via: Email: TNyitati@gmail.com or Mobile +255 (0) 718 471 318. He lives in Dar es Salaam but started his activities in Kilombero, Morogoro.

Written by simbadeo

June 20, 2010 at 2:40 pm

Posted in Siasa na jamii

Kibaha …

leave a comment »


Utokapo Dar.

Mto unaotenganisha mikoa ya Dar es Salaam na Pwani

Wapo waliogonga kingo za daraja … na hakuna marekebisho yaliyofanyika … yaelekea ni muda mrefu umepita tangu ugongaji huo ufanyike. Hali hii huonekana mahali pengi … hatufanyi marekebisho ya sehemu zilizoharibiwa … tunaziacha kwa muda mrefu kiasi kwamba tunapozikumbuka … gharama za kurekebisha zinakuwa juu kiasi kwamba pengine ni vema kujenga upya kabisa. Tujirekebishe.

Written by simbadeo

June 20, 2010 at 12:24 pm

Posted in Siasa na jamii

Biashara…

leave a comment »


Biashara ndogondogo eneo la Karume jijini Dar es Salaam. Hapa imejaa mitumba ya nguo, viatu, mikanda, mabegi n.k. Lakini pia pamejaa bidhaa kibao za bei rahisi ambazo ni medi in chaina. Sijui lini tutakuwa tukiuza bidhaa zilizozalishwa hapa hapa nchini.

Written by simbadeo

June 20, 2010 at 12:13 pm

Posted in Siasa na jamii

Shirika la Elimu Kibaha …

leave a comment »


Shule ya Sekondari Kibaha – moja ya shule bora nchini.

Maktaba ya Umma – Kibaha

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Jamii (Ufundi) – Kibaha, Bw. Baradyana. Chuo hiki ni sehemu ya Shirika la Elimu Kibaha.

Tumbi Hospital. Ni sehemu ya Shirika la Elimu Kibaha.

Lengo la kuanzishwa kwa Shirika hili la Elimu Kibaha ilikuwa ni kutengeneza modeli ya taasisi zenye lengo la kutokomeza maadui wakubwa watatu wa nchi yetu ya Tanzania, yaani, umaskini (kupitia utoaji elimu ya ufundi inayowawezesha vijana kujiajiri na kujitegemea), maradhi (huduma za afya kupitia hospitali ya Tumbi) na ujinga (kupitia shule ya msingi ya Tumbi na Shule ya Sekondari ya Kibaha na nyinginezo zilizo hapo). Kulikuwa na bado zipo shughuli nyingine nyingi zinazoedeshwa chini ya Shirika hili.

Pengine ni wakati sasa Serikali yetu iendeleze nia ya kuanzishwa kwa Shirika hili – kwanza ianze na kuliimarisha shirika hili ambalo sasa baadhi ya miundo mbinu yake imeanza kuchoka. Pili, kila mkoa uanzishe Shirika la aina hii ili kuendeleza vita dhidi ya maadui wetu wakuu watatu, na sasa yupo adui wa nne – ufisadi – huyu naye hatuna budi kumpiga vita na kumshinda. Mikoa ipewe malengo ya kuwa imeanzisha taasisi za aina hii ndani ya kipindi cha miaka 10 ijayo. Inawezekana. Kupitia sera ya Kilimo Kwanza, taasisi kama hii inaweza kuleta aina ile ya mageuzi ya kimaendeleo tunayotaka kuleta nchini.

Written by simbadeo

June 20, 2010 at 11:38 am

Posted in Siasa na jamii