simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Slavery …

leave a comment »

Utumwa ungalipo. Utegemezi wa Afrika kama unavyojieleza katika picha ya pili kutoka blogu ya Bw Zitto Kabwe ni ishara tosha ya uendelezaji wa utumwa barani Afrika katika sura nyingine. Harakati za mwanamapinduzi, Martin Luther King, bado zinahitajika sana hata kama leo hii pale White House Marekani ameketi Rais mwenye asili ya Afrika. Makisio ya bajeti iliyotangazwa Alhamis wiki iliyopita yanadhihirisha utegemezi wetu, yanadhihirisha jinsi gani bado hatufanyi juhudi ya kutosha kuondokana na utumwa huu. Nchi na bara letu la Afrika viko katika kipindi cha mpito. Ni kipindi cha kufunga mkanda. Ni kipindi cha kujinyima ili vizazi vyetu vitakavyoishi miaka 200 mbele viwe vizazi huru, vizazi visivyotegemea ‘mjomba’ yeyote duniani, vizazi vyenye kauli kamili juu ya maisha na masuala yanayowahusu. Hatuna budi kulitambua hili. Salamu kwa Waheshimiwa sana Wabunge wa Bunge letu Tukufu lenye anwani yake kule Dodoma.

Advertisements

Written by simbadeo

June 14, 2010 at 9:54 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: