simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Pope Benedict XVI …

with 2 comments

Itakapofika Ijumaa tarehe 16 April, atatimiza miaka 83.

Lakini, skandali za ngono zinazowakabili mapadre mbalimbali hasa kule Ujerumani katika jimbo alilowahi kuongoza kama Askofu zinazidi kusababisha watu kumchimba.

Bila shaka ni wakati mgumu kwake na viongozi wenzake wa Kanisa hilo lenye waumini wengi zaidi duniani kuliko lingine lolote. Waumini pia watakuwa katika wakati mgumu kwa kunyoshewa vidole na waumini wa madhehebu mengine kwamba kwa nini waendelee kubaki katika kanisa ambalo limegubikwa na shutuma nzito hivyo?

Imani. Imani ni jambo gumu sana. Usidharau imani aliyonayo mtu mwingine. Wewe heshimu imani yake na yeye aheshimu imani yako. Hapo kutakuwepo amani. Imani. Imani ni imani tu – inaelekezwa kwa Mwenyezi Mungu – si kwa binadamu wala kupitia kwa binadamu. Kwa hiyo, vitendo vya mwingine havipaswi kukwaza imani ya mtu LABDA kama imani hiyo mtu ameifunga kupitia kwa binadamu mwingine – jambo ambalo mimi siamini kama ni sawa. Unamwamini MUNGU tu. Ishi imani hiyo.

Hii si kuwatetea mapadre, la hasha, waliofanya vitendo hivyo wachukuliwe hatua za kisheria ili haki itendeke. Makosa yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa yaadhibiwe kama inavyostahili. Utoaji adhabu huu usichague huyu ni maskini, huyu ana mamlaka, huyu ni hivi, huyu ni vile. Wazee wetu wa Kiswahili walipata kusema: ‘Bata ukimchunguza sana, humli’. Kwa hiyo, ukianza kupekenyua pekenyua kuhusu imani yoyote iliyo chini ya jua – hutaila (hutaipokea) maana utakayoyakuta huko – au kwa agents wa imani hiyo – vitakukera kama si kukutapisha kabisa.

Link kutoka yahoo kuhusu habari ya Papa:

http://news.yahoo.com/s/ap/20100411/ap_on_re_eu/eu_pope_s_ivory_tower

Advertisements

Written by simbadeo

April 12, 2010 at 10:18 am

Posted in Siasa na jamii

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. i didnt know that we share the same date of birth. At least i have learn from u. Thanks

  Like

  wacuka44ew

  September 25, 2011 at 4:45 pm

 2. Congratulations Wacuka. This means you too share his ‘popeliness’ … Well, such is life.

  Like

  Deo Simba

  September 25, 2011 at 5:20 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: