simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Ajira … kwa/za vijana

leave a comment »

Tazama picha hizi hapa chini:

Kuna tofauti kubwa.

Wa mtu katika picha ya kwanza ni mchuuzi wa bidhaa ambazo zimetengenezwa nje ya nchi. Yeye hajatia ubunifu katika kazi hiyo … labda katika manjonjo ya kuuza. Kiufupi anawafanyia biashara wale waliotengeneza kwa maneno mengine biashara  kama hii inakuja kuchota ‘tudola’ tuchache tunachotuma kwa kuuza kahawa, katani, pamba, samaki, madini n.k.

Huyo wa pili anaketi chini (au kuna mtu hapa hapa nchini anayeketi chini) na kutengeneza mabango hayo yenye picha. Kisha anaingia mtaani kuyachuuza. Kwa maana hiyo anaipa hela yetu ya ‘madafu’ fursa ya kuzunguka hapahapa nchini.

Hizo picha zilizobaki ni vijana wanaoendesha vitalu vya miche ya miti. Wanapouza miche hiyo nao pia wanasaidia hela yetu ya ‘madafu’ kuzunguka hapa nchini pasipo kukimbilia nje ya nchi.

Kwa ulinganisho huu … je ajira za vijana zichukue njia ipi kati ya hizo hapo juu? Kwa maoni yangu: ajira za vijana hazina budi kuakisi (reflect) ukuzaji wa vipaji vya Watanzania. Ajira hizo hazipaswi kuwa zile zinazotugeuza wachuuzi wa ubunifu na material ya wenzetu wa huko ng’ambo. Tule tunavyotengeneza hapa kwetu … vile vitakavyosaidia kujenga uchumi wetu na si kuuangamiza.

Advertisements

Written by simbadeo

April 10, 2010 at 6:32 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: