simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Segerea … mwisho

leave a comment »

Ni katika pitapita zangu. Nilifika Segerea Mwisho. Kuna stendi nzuri ya mabasi ya daladala iliyojengwa miezi ya karibuni. Nasema ‘nzuri’ kwa lugha ya kilei. Maana mie sio mtaalamu wa ujenzi wa barabara na miundo mbinu ya aina hiyo. Ila kwa macho stendi hiyo inaonekana kuwa nzuri. Kilichonivutia zaidi ni wazo la kujenga stendi kama hiyo kwa ajili ya kitongoji cha Segerea na vile vya jirani kama kule Kinyerezi. Nafikiri stendi hizi zingejengwa kwa wingi zaidi katika jiji la Dar es Salaam ili kupunguza mabasi ya daladala yanayopaki barabarani wakati wa kushusha nakupakia abiria. Inawezekana.  Itabadilisha sura ya jiji. Italipa mvuto zaidi.

Kingine. Haitoshi tu kujenga stendi kama hizi. Inafaa pia kufikiri namna gani miti na maua vitapata nafasi katika stendi hizo. Hapa sioni miti itapandwa wapi. Miti husaidia sana katika kupendezesha mandhari ya eneo. Lakini pia husaidia kwa suala la kivuli na hali ya hewa ya eneo. Inafaa pia kuweka mapipa ya kutupia takataka kwa wingi. Maana baada ya muda eneo hili litaanza kujaa uchafu wa kila aina. Kumbe basi: stendi zijengwe kwa wingi zaidi jijini Dar. Miti na maua vipate nafasi. Suhula za kutupia takataka ziwekwe kwa wingi. Kwa ujumla hongera waliobuni na kujenga stendi hii.

Advertisements

Written by simbadeo

April 9, 2010 at 11:20 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: