simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Ndala…Igunga … ni Tanzania

with one comment

Tanzania ni nchi kubwa. Kuna vitongoji, vijiji, mitaa, miji na majiji. Mambo mengi yanafanana toka eneo moja hadi jingine. Lakini lililo kubwa zaidi ni pamoja na mchango wa taasisi za kidini katika kutoa huduma. Kuna hospitali nyingi tu zilizoanzishwa na taasisi za kidini. Mchango wake katika kutoa huduma kwa jamii hauwezi kupuuzwa. Tuone taswira hizi mbili.

Hapa panaitwa Ndala. Taswira hii utaikuta mahali pengi nchini Tanzania. Sehemu ya kilaji (kinywaji), chips na kijiwe cha kubadilishana mawili matatu. Hii ilikuwa ni majira ya saa 9 au 10 hivi. Labda swali la uchokozi, hivi tunafanya kazi saa ngapi ili tuzalishe kiasi cha kutosha kuvuta starehe namna hii? Kwa mtindo huu nchi itaendelea? Ni swali la uchokozi.

Ni Hospitali Teule ya Nkinga huko Igunga. Ilianzishwa na Kanisa la Pentekoste. Tunaona hapa mchango wa taasisi za kidini katika kutoa huduma za jamii. Ni vizuri tuendeleze mshikamano wa aina hii. Hata kama tuna imani tofauti bado tunaweza kuwa majirani wema na kuishi bila kubaguana. Jambo hili ni kubwa kwetu Watanzania na hatuna budi kujivunia. Tumesikia jinsi ilivyo jambo gumu kwa WaNigeria kuishi pamoja watu wa imani tofauti. Inasikitisha. Inatupa funzo kwamba tusipoteze tunu hii tuliyo nayo. AMANI idumu Tanzania.

Advertisements

Written by simbadeo

March 11, 2010 at 2:53 pm

Posted in Siasa na jamii

One Response

Subscribe to comments with RSS.

 1. NIMEFURAHI SANA KUONA MAENEO YA NYUMBANI,
  NAKUBALIANA NA WEWE KWAMBA WATU WANAKAA BILA KUFANYA KZ MUDA WA KAZI, MIMI NAFIKIRI KIPINDI ULICHOENDA NI KIPINDI CHA KIANGAZI! KIPINDI AMBACHO WATU WANAKUA WAMESHAVUNA MAZAO YAO, MAANA WATU WA KULE WENGI NI WAKULIMA.LKN KAMA UNGEENDA KIPINDI CHA MASIKA
  HAKIKA USINGEWAKUTA WATU WAMEKAA TU MUDA WA KUFANYA KAZI.
  KARIBU SANA NDALA,
  MUNGU AKUBARIKI

  Like

  longino masanja.

  September 30, 2011 at 4:40 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: