simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mwese…Mpanda

with 66 comments

Miaka 30 imepita tangu nilipokanyaga Mwese… mahali nilipozaliwa. Ni kipindi kirefu. Ilikuwa furaha kubwa kufanya tena ‘reunion’ na eneo hilo pamoja na ndugu na jamaa. Safari zangu zilikuwa zikinifikisha mpaka Mpanda mjini tu. Lakini safari hii nilipata fursa ya kufika Mwese. Mwese, ooh Mwese, Mwese nitarudi tena! Inanikumbusha nyimbo ile ya ‘Mwanza’. Baadhi ya picha za Mwese ni hizi:

Ni katika barabara ya kwenda Mwese. Misitu ya asili iliyoshona vizuri inapendeza sana.

Mdogo wangu niliyefuatana naye, Imanuel, akipanda kilima cha kwenda dispensary ya Mwese.

Mwese kutokea eneo la juu kidogo.

Shule ya Msingi ya Mwese – wapo wengi sana waliopita hapa – hasa ndugu zetu Wanyarwanda waliopata kuishi Mwese miaka ile ya kuwa uhamishoni.

Kahawa na migombo ni baadhi ya mazao yanayostawi vema huko Mwese.

Ujenzi wa moja ya madaraja katika barabara inayounganisha Mpanda na Mwese.

Bibi yangu, Wajombwe, mwenye zaidi ya miaka 90 akiwa na bwana mdogo Immanuel. Kiswahili cha bibi kimenyoka vizuri tu ila meno karibu yote hana, lakini bado yu madhubuti.

Ilikuwa safari nzuri sana. Mungu akijaalia uzima nitakuwa nafika walau mara moja kila baada ya miaka 2.

Written by simbadeo

March 5, 2010 at 3:10 pm

Posted in Siasa na jamii

66 Responses

Subscribe to comments with RSS.

  1. Nafurahi sana kuona picha za mwese kwenye mtandao. Imenikumbusha mbali sana kwa sababu ndo sehemu niliko zaliwa (mwese No. 3).

    Like

    Baptist Kagarama Christian (Gatiritiri)

    January 11, 2011 at 1:09 am

    • Ndugu Baptist,

      Nimefurahi sana kwamba umefurahia picha nilizoweka kwenye mtandao. Nikipata fursa nyingine ya kutembelea tena Mwese, nitakuletea picha nyingi zaidi. Na nafikiri sasa hivi nafahamu nini hasa watu waliopata kuishi na kuifahamu Mwese wangependa kuona. Kila la kheri na tuzidi kuwasiliana hata kwa barua pepe. Wasalamu, Deo Simba.

      Like

      simbadeo

      January 11, 2011 at 11:52 am

  2. Mwese ni kama nchi ya Ahadi naomba ufike japo cku moja hapa mwese sec. uwashawishi nduguzo umuhimu wa shule bado wamelala. Wanashule nzuri umeme upo hadi hosteli lakini wamelala INATUKATISHA TAMAA WALIMU.Nimehuzunika ht picha moja ya sekondari hujaiweka noma hiyo kaka.

    Like

    Mwalimu

    January 23, 2011 at 10:15 pm

  3. nimefurahi sana kuona picha za mwese sababu nimahari ambapo nimererewa,nasikitika sana na kuona hospital,sijuwi jinsi nirivyo iona kwenye picha kwa mbari kama ndivyo irivyo!watanzania jamani mjenge hospitali yenu hapo mwese?(mutange umuganda)mbona majengo ya shule yameharibika kweri naumuia sana ila mwenyezi mungu awasaidie,ivi nasi twajenga nshi yetu rwnda

    Like

    innocent rutangusa

    January 25, 2011 at 3:47 am

    • Ndugu Innocent, asante sana kwa maoni yako. Ni kweli kwamba hali ya hospitali ya Mwese si nzuri kwa ujumla. Huduma imekuwa hafifu na majengo yamechakaa. Wakati huohuo vifaa vya kutolea huduma ya tiba navyo ni vya shida au ni vichakavu sana. Ama kwa hakika hatuna budi sisi Watanzania na wengine wenye mapenzi mema kurejesha hadhi ya hospitali hii kuwa iliyokuwa ya kutoa huduma bora. Tunawapongeza ninyi huko Rwanda, nasikia kwamba mnapiga hatua kubwa kubwa za maendeleo … tunawapongeza sana. Nakutakia kazi njema za ujenzi wa Taifa lenu lakini pia ujenzi wa Afrika ya Mashariki. Tafadhali tembelea mara nyingi zaidi blogu hii. Naamini kuna chochote utakachopata cha kujifunza. Kila la kheri. Wasalimu woote waliowahi kuishi kule Mwese.

      Like

      simbadeo

      January 25, 2011 at 2:30 pm

  4. Napenda kuona picha ya Mabisye nilipokuwa napenda kuchungia nk’ombe. Fanya ukirudi upublish picha ya Amrani, Makokoto na Kapegu (No.3).Mwese oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    Like

    Kagarama J. Baptist

    January 25, 2011 at 10:54 am

    • Ndugu Kagarama, asante kwa kutembelea blogu hii. Ninakuahidi kwamba mara nipatapo nafasi ya kufika Mwese, nitakuletea picha za kule, safari hii nitapiga picha nyingi zaidi na katika maeneo mbalimbali. Salamu kwa wengine wote huko.

      Like

      simbadeo

      January 25, 2011 at 2:27 pm

    • Hee Baptist umemsahau rafiki yetu Festus Joram wa no 9 ila mi ningependa kumuona pia mtu yeyote kutoka familia ya Mr Husein Kajenje wa no 10. Juma Husein, Yusuph Husein Kajenje au hata Mr Miraji. Ningefurahi sana.

      Like

      Hassan Rugwiza

      March 4, 2012 at 10:28 pm

      • Ndugu Hassan, asante sana kwa kutembelea blogu hii. Nitatafuta picha ya baadhi ya wanafamilia wa Kajenje walio hapa Dar ni kuwawekea hapa. I hope hawatakuwa na neno. Nitawafikishia salamu pia kutoka kwako.

        Nipatapo tena safari ya Mwese, nitafanya juhudi zaidi ili kuwaletea picha za kina za kila kona kwa ajili ya kumbukumbu zenu na kuona ninyi pia mtasaidia vipi kuinua hali ya maisha ya watu wa Mwese, mahali mlipokulia na kuanza maisha yenu, popote mlipo katika ulimwengu huu. Asante sana.

        Like

        simbadeo

        March 5, 2012 at 12:43 am

      • Ndugu Hassan habari za kazi. naitwa Fred kutoka Arusha. Bado hujamuona bwana Yusuph Kajenje? Nilikuwa naye Tabora pamoja na bwana John Shofeli. Habari pamoja na picha za Mwese kutoka kwa Deo zimenikumbusha mbali sana. Kazi njema kaka.

        Like

        FRED PROSPER TARIMO

        March 24, 2012 at 12:21 pm

      • Hi Fred. Karibu katika uwanja huu. Ni furaha kusikia kwamba ulikuwa na Yusuph kule Tabora. Inshaallah, panapo majaaliwa … blogu hii itawakutanisha tena. Endelea kuwa karibu.

        Like

        simbadeo

        March 24, 2012 at 11:58 pm

      • Hi, Jennifer. Nitakupigia. Asante kwa nambari yako ya simu. Unaweza pia kuniandikia email kupitia kakasimba@gmail.com

        Kila la kheri.

        Like

        simbadeo

        March 26, 2012 at 8:04 pm

  5. ok aksaza aksnte sana lakini naomba utupatiye picture kwa hufahamu zaidi kwa hiyo itanifurahisaha kwa kupata maendereowo yetu

    Like

    innocent rutangusa

    March 3, 2011 at 2:33 pm

    • Ndugu Innocent,

      Asante sana kwa maoni yako. Sijapata tena fursa ya kurudi Mwese. Hata hivyo, mara nitakapofanya hivyo, nitahakikisha ninapata picha za maeneo mbalimbali pale Mwese n kuwawekea hapa wadau wote. Tuvute subira. Sijafahamu bado ni lini nitafika kule Mwese … lakini kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu nitafika. Endelea kusoma habari mbalimbali zinazokujia kupitia blogu hii.

      Kila la kheri.

      Like

      simbadeo

      March 3, 2011 at 2:56 pm

  6. Aise nashukuru sana kwa kupata habari na baadhi ya picha za mwese, naomba picha ya baadhi ya nyumba za No 1 manake ndo turikozaliwa bwana, na tunapapenda sana.shukran.

    Like

    Burusu Raymond

    May 21, 2011 at 7:50 pm

  7. pia nami nashukuru sana kwani nimekumbushwa sehemu nilipo pata elimu yangu ya awali lwega primary school No 7.piga picha tu angalu moja ya shule yangu nitafurahi sana.ubaikiwe

    Like

    MASABO Alphonse. box kigali-rwanda

    July 25, 2011 at 4:52 pm

  8. Nimeona picture zimenikumbusha nilipokuwa mdogo. Mimi mwenyewe naisha Uingereza nilipo mweleza mama kuwa nimeona picture za mwese hakuniamini. Asante sana kwa kuweka hizo picture.Baptiste ulaho ulakomeye?.

    Like

    Kamanayo miss

    January 17, 2012 at 8:18 pm

    • Hello Kamanayo. Nami nimefurahi kwamba picha hizo zimekukumbusha mbali. Mwese ni eneo muhimu sana kwa watu wengi. Pamoja tushirikiane kuona tunaenzi vipi Mwese iliyotulea, Mwese iliyotupa maisha tuliyo nayo hivi sasa. Waweza kuwasiliana nami kupitia kakasimba@gmail.com kwa maoni na fikra zaidi. Asante na endelea kutembelea blogu hii. Mungu akijalia, siku nikienda tena Mwese, nitaweka picha zaidi hapa.

      Like

      simbadeo

      January 18, 2012 at 1:09 am

      • Hey we ndugu unatukumbusha mbali hasa unapo tuonyesha picha za mwese. kweli ipo siku tutakuja kutembelea mwese. wengi tunaifahamu kama mexco. Angali hiyo shule ya msingi mwese .wengi tumepitia hapo ndo msingi wa maisha yetu. Hassan Rugwiza

        Like

        Hassan Rugwiza

        March 4, 2012 at 10:20 pm

    • Yaani akiweka zile za kule juu ndahangwa ndo utafurahia kabisa.

      Like

      Hassan Rugwiza

      March 4, 2012 at 10:30 pm

    • Simba Deo! bado tu hujarudi mwese uweke pics ningine kama urivyoahidi?Kamanayo miss, amakuru y’imyaka myinshi?suhuza umugabo n’abana

      Like

      Baptist

      August 3, 2012 at 1:33 pm

      • Ndugu Baptist. Nilipata saa chache za kufika Mwese. Niliingia saa sita mchana na kuondoka saa 12 jioni. Ninapandisha picha chache mpya nilizopata kwa muda huo mfupi. Nilikuwa na watu wengi wa kuonana nao na sikufaulu kufika kila mahali. Bila shaka unaona kwamba picha ninazoweka siku hizi zinaonyesha majira ya kiangazi na zile za wakati ule ilikuwa masika. Karibu uendelee kutembelea blogu hii kwa picha nitakazokuwa nikiweka hapa. Asante.

        Like

        simbadeo

        August 3, 2012 at 10:53 pm

  9. Hello Their, Kusahau ulikatoka nimakosa, nilipo kiona kituo cha afya cha zamanisana mwese nikamkumbuka pia muuguzi: MALIANA, shule zote za msingi zilizotulea,pia vijiji vyote vilivyo tuhifadhi, bila kusahau KARUKUMBA: Hapo ndiponilifanyia kazi ya ku choma:MUKAA. Asubuhi shuleni na gunia la mukaa kichwani: Bila kusahau watu muhimu sana walio tulea na kutupatia elimu ya msingi,niwezao kuwakumbuka ni: Mwalimu: I Gahamanyi, Fataki, J Bisetsa, Emmanuel, Margrete Karuletwa,Shofeli,Flavia Kirimanzira, Mpagalala,Gatari,Kayumba,Tadeo.nawengineo ambao sikuweza kuwa kumbuka, all of them deserves HONOUR. This is Just ajoke:Tusyesye, ulimpola mujango, kupanga kulugo mujango.UDUMU, UMOJA WA RWANDA NA TANZANIA, NA UDUMU MUUNGANO AFRIKA MASHARIKI: na ( MUNGU AMREHEMU MAHALI PEMA PEPONI: MWALIMU: JULIAS KAMBALAGE NYERERE) nimi wenu katika kumbukumbu:EDWARD NGOGA ( KIHOKONYORO)From uk,Oxford.

    Like

    Edward Ngoga

    March 10, 2012 at 7:00 pm

    • Karibu sana Edward Ngoga. Kama unavyosema, tukumbuke tulikotoka.

      Like

      simbadeo

      March 11, 2012 at 12:41 am

    • Andika walimu walio kufundisha. Naona unaandika walimu wa Kinyarwanda tu. Na tena muchanganyiko. Wewe ulisomea shule za msingi zote? Wanyarwanda wengi walisomea sehemu tofauti tanzania sasa kuwa mstaalabu Edward Ngoga. Andika shule uliyeyo somea kisha walimu walio kufundisha halafu shukuru wengine wote tanzania ukitaka uwataje kama walimu ambao hawakufundisha lakini uliwajua.

      Like

      Bigwa

      February 7, 2013 at 4:04 pm

  10. Mr Simba hongera sana kwa kuiweka mwese kwenye mtandao!next time ufike na Lugonesi especially no,4.kweli wewe ni mzalendo wa kweli.Naamin kupitia kwako we can organise something for mwese!God bless you!!!!!!

    Like

    Alex John [Lingi]

    March 14, 2012 at 10:43 pm

  11. ooo my God! nimefurahi sana kwasababu hizi picha zimenikumbusha bali sana!!!
    jamaani picha nyingi zinahitajika.
    Grace Dusa

    Like

    Grace Dusa

    March 15, 2012 at 1:07 pm

    • Karibu sana Grace. Mungu akubariki kwa kuguswa na mahali hapo. Ni wengi tuna historia na eneo hilo. Karibu sana. Mungu akijaalia, tutapata picha zaidi.

      Like

      simbadeo

      March 21, 2012 at 11:38 pm

  12. Ndugu Alex. Asante sana. Asante kwa simu. Naamini huu ni mwanzo mzuri. Tuliendeleze jambo hili. Kila la kheri.

    Like

    simbadeo

    March 21, 2012 at 11:39 pm

    • Mungub wangu, Mwse…..Niliishi miaka ya 1975 hadi mwaka 1980……Napakumbuka hasa shule ya msingi kulikuwa na mabaki ya kichwa cha ndege ilidondoka pale…Bado kipo jamani wa huko???

      MTOTO WA MZEE KISINZA.

      Like

      Gasper Tryphon Kisinza

      March 24, 2012 at 12:29 pm

  13. TUNAOMBA PICHA ZAIDI ZA MWESE….VILIMA NA MTO KAMA WAINGIA KIJIJINI, KANISA LA RC, MAJENGO YA SHULE NA HATA BAADHI YA WALIMU WA MSINGI WA WAKATI WA MIAKA YA 1980S…….JAPO WAKATI HUO NILIKUWA NA MIAKA MITANO TU…..

    Like

    Gasper Tryphon Kisinza

    March 24, 2012 at 12:31 pm

    • Ndugu Gasper, asante sana kwa maoni/mapendekezo yako. Panapo majaaliwa … tutapata picha zaidi. Tupo pamoja. Deo Simba.

      Like

      simbadeo

      March 24, 2012 at 11:56 pm

  14. Salaam kwa watu wote wa mwese. Kweli kaka simba wewe unaweza kutukumbusha na kutukutanisha wadau wote wa mwese. mungu akubariki sana. kaka Fred kweli kama unaonana na Yusuph Kajenje mpe salaam zangu. ndugu kisinza wewe ulikuwa jirani no 3 Mungu awabariki wote.

    Like

    Rugwiza Hassan. ( Hassan Ismail)

    April 1, 2012 at 11:09 pm

    • Simba Deo! bado tu hujarudi mwese uweke pics nyingine kama urivyoahidi?Asante sana Hassan kunikumbusha Yusuf Kajenje. Nataka kujua kama ile miwa ya kwa mzee Kajenje no.10 bado ipo.

      Like

      Baptist

      August 3, 2012 at 1:32 pm

      • Hi Baptist! Ulaho? Ndakomeye Cyane! Ndugu yangu ile miwa kule No 10 bado ipo. Karibu sana

        Like

        Yussuf Kajenje

        December 6, 2012 at 1:03 pm

      • Ndugu Kajenje … yaani umenifanya nipate hamu ya kwenda tena Mwese. Safari ijayo nitahakikisha ninakaa walau wiki nzima ili nami nifaidi miwa hiyo.

        Like

        simbadeo

        December 7, 2012 at 12:41 am

  15. ohoooooo mwese our promised land………………………

    Like

    munyandamutsa Eudes

    September 30, 2012 at 8:25 pm

  16. Loo! mungu wangu wee!sijui niseme nini kweli!jamani,nianzie wapi niishie wapi?simba mungu akujalie snaa!kutukumbusha mwese!hivi mimi yapata miaka 20 sasa!jamani napakumbuka mno!SALEH SELEMANI

    Like

    nkusi saleh

    October 27, 2012 at 8:33 pm

  17. Ohh Mwese Lwega ndo nyumbani……. Na miss Mwese yetu oneday yes nitafika

    Like

    Nepo

    November 11, 2012 at 7:29 pm

    • ohho! mungu wangu nimefurahi sana kuona picha hizi kwasababu zimenikumbusha mengi kuhusu nchi yetu ya kuzariwa mwese oyeeeeeeeeeeeeeeee naomba mungu niweze kufika mwese angaru mara moja tu,

      Like

      ERNEST

      November 13, 2012 at 5:09 pm

    • Karibu Nepo. Yes, one day yes.

      Like

      simbadeo

      November 13, 2012 at 7:23 pm

  18. Nafurahi sana kuona tena nilipo zaliwa.wana mwese,tusisahau tuliko toka.God bless u all

    Like

    KAGARAMA ANGELUS

    December 14, 2012 at 1:05 pm

  19. Mzee,umenikumbusha mengi.Ukirudi mwese jaribu kurusha picha ya mlima wa mabishe.Nategemea mantonga na ntarari mengi sana.

    Like

    KAGARAMA ANGELUS

    December 14, 2012 at 1:09 pm

  20. simba DEO,Mungu akubariki kwa ujasili ulio nao.wewe una ishi wapi?na mimi nategemea
    kufanya tour Mwese.

    Like

    KAGARAMA ANGELUS

    December 14, 2012 at 1:17 pm

    • Ndugu Kagarama Angelus, asante sana kwa michango ya mawazo uliyotoa kwenye blogu yetu hapa. Mimi naishi Dar es Salaam. Unaweza kuniandikia kwa email kakasimba@gmail.com kwa miadi na mengineyo.

      Ukipata fursa ya kufika Mwese … itakuwa jambo la busara sana. Utapa kumbukumbu nzuri na kuona changamoto zinazowakabili ndugu zetu kule.

      Asante sana.

      Like

      simbadeo

      December 15, 2012 at 4:41 pm

  21. Nawakumbuka vijana tulio soma nao ambao bado wako mwese kama Ruvunja Kisaka,Zabron kutoka no 10,Hamisi Jombwe,Salum,Neema Mashaka,etc

    Like

    KAGARAMA ANGELUS

    December 14, 2012 at 1:21 pm

  22. Mwese oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, nawakumbuka sana watu wa mwese Kide na ndugu zake wote pia nawasalia sana wazazi wetu Mzee Philipo, Kisaka na wendine wote Mungu awarinde pamojya na Familly zenu zote.

    Like

    Epiphania Francis Nzaramba

    February 11, 2013 at 6:12 pm

  23. Lwega oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, kidumu chama chamapinduzi kidumufirakira za wananchi wa ccm CADEMA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

    Like

    MUGE.....

    February 13, 2014 at 6:26 pm

  24. CHADEMA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

    Like

    MUGE.....

    February 13, 2014 at 6:27 pm

  25. Naona wenzangu mmekuwa kimya sana. Simba Deo hujambo na ndugu zangu wengine hamjambooooo???

    Like

    Kagarama Baptist

    September 12, 2014 at 7:19 pm

    • Habari zenu wote! nami nimefurahi sana kuona picha za Mwese Meksico City ni miaka mingi tangu nilipotoka huko lakini naomba Mungu anijalie nipate tena frusa ya kufika tena.Nimewakumbuka jamaa na marafiki waliobaki huko Mungu awrinde wote.ni Damasceni RUTOKI Aksante sana.

      Like

      RUTOKI Damascene

      January 1, 2015 at 1:25 am

  26. SIMBADEO SHUKURANI.

    Simbadeo shukurani,
    kwa dhati toka moyoni,
    kusahau masikani,
    si uungwana asilani.

    Mwenyi enzi Maulana,
    Mwese ibariki sana,
    wafanye waMwese wana,
    daima kuelewana.

    Tufikiri kwa pamoja,
    kujadili hii hoja.
    ya nani anayo haja?
    ya jenga Mwese umoja.

    Mola wetu tuwezeshe,
    njozi zetu ‘kamilishe,
    jamii yetu ‘jumuishe,
    MWESE tuiendeleshe.

    John Jacob KAGARAMA (Janjaki)
    Mwana wa Mwese.

    Like

    Rwaka rwa Kagarama

    November 16, 2015 at 1:06 pm

    • Shukrani sana Ndugu Rwaka rwa Kagarama kwa shairi makini. Nimehemewa. Kikubwa nachoweza kusema ni ‘asante sana’. Pamoja sana katika kuienzi Mwese yetu. Itabaki kuwa na umuhimu wa pekee kwetu sote.

      Pamoja.

      Deo Simba

      Like

      simbadeo

      December 1, 2015 at 6:58 pm

  27. Uuuuh !!! Yaonekana kuwa habari hii imesuuza nyoyo za wengi, hususan walozaliwa na kukulia Mwese.
    Bwana SIMBADEO astahili shukurani kwa sababu habari yake imekuwa chachu ambayo imeamsha na kugusa sana nyoyo kwa kuwakumbusha wengi, eneo ambalo lina upekee katika maisha yao nami nikiwemo. Eneo ambalo vitovu vya walio wengi kutoka MWESE vilizikwa walipozaliwa, mathalani, wengi nilowaona hapa wamezaliwa katika zahanati ya Mwese yenye picha inayopatikana ktk moja ya habari za blogu hii (hata mlango wa chumba cha wakunga kipindi hichoooo naukumbuka. Ni Mlango wa tatu kutoka kushoto). Eneo ambalo ardhi yake imehifadhi miili ya mababu, wazazi na ndugu kwa baadhi ya wale walioishi huko. Bila shaka hii ni ardhi takatifu.

    Natamani sana habari hii ambayo ni mbegu ilopandwa katika ardhi yenye rutuba (utandawazi), ikuwe na kuzaa tunda la UMOJA miongoni mwa wanaMwese, kwamba siku moja Mwenyi enzi Mungu atuwezeshe, bega kwa bega kutoa mchango kwa namna moja au nyingine katika maendeleo ya Mwese, hususan maendeleo kitaaluma au kuichangia sekta ya tiba.

    Hayo ni maoni yangu, Tafadhali nawe utoe maoni yako mwanaMwese.

    A HUMAN BEING WAS CREATED TO TRANSFORM THE WORLD, AND THE WORLD STARTS AT HOME.

    Like

    Rwaka rwa Kagarama.

    November 16, 2015 at 2:59 pm

  28. Nimeriwadhika vilivyo kwamba mwandishi ambaye naamini kuwa sikujidanganya kufikiri kwamba ana taaluma kujumlisha kipaji, amenipata.
    Bwana Simba Deo, Mwenyi enzi akujalie kheri, na ikiwezekana upige hatua zaidi na zaidi kila upatapo nafasi ya kuwasiliana na wana Mwese kwa pamoja , kwa kuutumia utandawazi, kwa sababu wewe ni kijana ambaye naona waweza kuwa na mchango mkubwa sana kuwaweka pamoja wana Mwese ili siku moja tuipatie mwese mchango KWA PAMOJA kama motto yako njema isemavyo.

    WAKATABAHU.

    Like

    Rwaka rwa Kagarama.

    December 2, 2015 at 4:01 pm

  29. KUKOSOWA: Samahani, naona MOTTO yako ni ni PAMOJA SANA si KWA PAMOJA kama nilivyoandika hapo juu.

    Like

    Rwaka rwa Kagarama.

    December 2, 2015 at 4:05 pm

  30. SHUKURANI KWA MOLA.

    SHUKURANI MUADHAMA, SUBUKHANA USWIFIKE.
    KUN’GEA HUU UZIMA, WANAMWESE MPULIKE.
    WANAKWETU MU SALAMA? WOTE WAUME NA WAKE.
    MOLA MWEMA MWELEKEZI, AWE NANYI SIKU ZOTE.

    HICHI KIPINDI MWAFAKA, KUKUMBUKA WALON’FUNDA.
    KUMSOMA BULICHEKA, KUHESABU MPAKA KENDA.
    NIKIKUMBUKA N’NACHEKA, SOMO LA KWANZA NIK’ENDA.
    MOLA MWEMA MTUNUKU, KULA ALIENIFUNDA.

    NDURU YANGU IPULIKE, NAIPAZA KWA TA’DHIMA.
    MUNGU WA SIFA ZA PWEKE. SIMBA MGEE UZIMA.
    DEO ANA UPEKEE, ASITAHILI HESHIMA.
    MOLA MWEMA MBARIKI, KUT’WEKA PAMOJA SANA.

    Like

    Rwaka rwa Kagarama.

    January 29, 2016 at 1:57 pm

  31. THAMANI YA UPOLE.

    1. Mwenzangu kaa kitako, 7. UPOLE una thamani,
    Upulikize tamko. Ni dhana bora jamani.
    Lisilo dhara na mwiko, Ni tuzo lake Manani,
    Ni lenye fanaka kwako. Kwa MPOLE muumini.

    2. Rai hii ni aghali, 8. UPOLE ninaoghani,
    Inaziduwa akili. Si ukimya eleweni.
    Ni tamko la ukweli. Si kuduwala jamani,
    Usio na mushikeli. Ni wa busara kichwani.

    3. Hichi cha thamani kitu, 9. Mkora mwizi hatari,
    Cha UPOLE mwanakwetu. Ni wa ukimya mahiri.
    Upole swifa ya utu, Uhasimu asitiri,
    Si sawa na utukutu. Si upole tahadhari.

    4. Matamko ya MPOLE, 10. Upole ni wa ushwari,
    Hayaji kimbelembele. Si ukimya wenye shari.
    Hadi matoye yalole, UPOLE wabeba kheri,
    Lipulike sikiole. Si ukimya wa hatari.

    5. MPOLE ntu mwafaka, 11. UPOLE una thamani,
    Fikiraze za fanaka. Ni dhana chanya jamani.
    Nenole lina baraka, Ee Mtajika Manani.
    Huwa limesawazika. UPOLE tujalieni.

    6. MWANAPOLE neno lake, 12. Ewe nawe mshairi,
    Si rahisi lifunuke. Towa wako ushauri.
    Mpaka uchambuzi wake, UPOLE wake usiri,
    Wa wazo ukamilike. ‘Tweleze kwa umahiri.

    Rwaka rwa Kagarama

    Like

    Rwaka rwa Kagarama.

    February 5, 2016 at 6:48 pm

  32. THAMANI YA UPOLE

    1. Mwenzangu kaa kitako,
    upulikize tamko.
    Lisilo dhara na mwiko,
    ni lenye fanaka kwako.

    2. Rai hii ni aghali,
    inazinduwa akili.
    Ni tamko la ukweli,
    Usio na mushikeli.

    3. Hichi cha thamani kitu,
    cha UPOLE mwanakwetu.
    UPOLE swifa ya utu,
    Siyo kana utukutu.

    4. Maneno ya MWENDAPOLE,
    hayaji kimbelembele.
    Hadi matoye yalole,
    Lipulike sikiole.

    5. MPOLE ntu mwafaka,
    fikiraze za fanaka.
    Nenole lina baraka,
    huwa limesawazika

    6. MPOLE tamko lake
    si rahisi lifunuke,
    Mpaka uchambuzi wake
    wa wazo ukamilike.

    7. UPOLE una thamani,
    ni dhana bora jamani.
    Ni tuzo lake Manani.
    Kwa mjawe muumini.

    8. Upole ninaoghani,
    si ukimya eleweni.
    Si kuduwala jamani,
    Ni wa busara kichwani.

    9. Mkora mwizi hatari,
    ni wa ukimya mahiri.
    Uhasimu asitiri,
    Si UPOLE tahadhari.

    10. UPOLE una ushwari,
    si ukimya wenye shari.
    UPOLE wabeba kheri,
    Si utulivu hatari.

    11. UPOLE una thamani
    ni jamvia la amani.
    Ee Mtajika Manani.
    WAPOLE wajalieni.

    12. Ewe nawe mshairi,
    lete wako ushauri.
    UPOLE wake usiri,
    tweleze kwa umahiri.

    RWAKA RWA KAGARAMA,

    RWANDA.

    Like

    Rwaka rwa Kagarama.

    February 11, 2016 at 2:19 pm

  33. Nakusalimu sana Bwana Simba pia wanaMwese kwa ujumla ambao wanaizuru blogi hii. Nasikitika tu kwamba, sasa hivi inaonekana hatuitumii vilivyo, ama kweli ” kwenye miti, hakuna wajenzi.”
    Sasa bwana Deo hapa chini ninakutumia ushairi huu, hususan kwa sababu nimemaizi kuwa wewe ni mpenzi wa Mashairi kama sikukosei.

    UTAMU WA MASHAIRI.

    1. Ni matamu mashairi, yana ladha siyo siri.
    Tamko hili dhahiri, kwake kula mshairi.
    Ubongo nikivinjari, utunzi kuufikiri.
    Ninahisi kana kwamba, ninailamba asali.

    2. Niziwazapo bahari, bahari za mashairi.
    Ka’malumbano shairi, hata mandhuma shairi.
    Zilotungwa na mahiri, malenga wa mashairi.
    Utamu wake hakika, nauhisi nafsini.

    3. Bahari ze zinakuwa, za aina maridhawa.
    Ni mithili ya mauwa, bustanini yatuwa.
    Maua yasiyo sawa, kwa rangi utavutiwa.
    machoni yana utamu, ya ladha kama shairi.

    4. Wa mashairi utamu, unakuwa akilini.
    Unapotoa elimu, kuijaza ubongoni.
    Ndani una utaalamu, kupitia usanii
    Ladha yake yahisika, sikioni na moyoni.

    5. Ni matamu eleweni, ukiyazamia ndani.
    Ukaonja saharani, ukara na sakarani.
    malumbano ye jamani, na sabilia amini.
    Ni bahari za shairi, ladha zake ni ajabu.

    6. Leo nakomea hapa, hauruhusu wakati.
    Kazi nyingine nachapa, Nina mingi mikakati.
    Shukrani Mola ‘menipa, kuifikia tamati.
    ya mishororo mwanana, ya utamu wa shairi.

    *****************

    RWAKA RWA KAGARAMA

    RWANDA..

    Like

    Rwaka rwa Kagarama.

    February 29, 2016 at 2:32 pm

  34. Salamu nyingi ziwafikie wanaMwese hususan Bwana Simba, mwanzilishi wa blogi hii, ambaye ni mpenzi wa mashairi. Wapenzi wengine wa fani hii ya kiswahili sijawafahamu, lakini naamini wapo, hivyo mguso na ladha ya tungo hilo hapo chini, ninaamini yatawafikia.
    Alhamdulilah.

    MASHAIRI NI MATAMU.
    ___________________

    1.Ni matamu mashairi, yana ladha siyo siri.
    Tamko hili dhahiri, kwa wapenda mashairi.
    Ubongo nikivinjari, utunzi kuufikiri.
    Ninahisi kana kwamba, ninailamba asali.

    2.Ninapowaza bahari, bahari za mashairi.
    ya malumbano shairi, hata mandhuma shairi.
    Zilotungwa na mahiri, malenga wa mashairi.
    Utamu wake hakika, nauhisi nafsini.

    3.Bahari ze zinakuwa, za aina maridhawa.
    Ni mithili ya mauwa, Bustanini yatuwa.
    Maua yasiyo sawa, kwa rangi utavutiwa.
    masoni yana utamu, wa ladha kama shairi.

    4.Wa mashairi utamu, unakuwa akilini.
    Unapotoa elimu, kuijaza ubongoni.
    Ndani una utaalamu, kupitia usanii.
    Ladha yake yahisika, sikioni na moyoni.

    5.Ni matamu eleweni, ukiyazamia ndani.
    Ukaonja saharani, ukara na sakarani.
    Malumbano ye jamani, na sabilia amini.
    Ni bahari za ‘shairi, zenye ladha ya ajabu.

    6. Leo nakomea hapa, hauruhusu wakati.
    Ipo kazi naichapa, yenye mingi mikakati.
    Shukrani Mola ‘menipa, kuifikia tamati.
    Tamati ya mishororo, ya mashairi matamu.

    ************************

    RWAKA RWA KAGARAMA

    MSHAIRI MNYARWANDA.

    Like

    Rwaka rwa Kagarama.

    February 29, 2016 at 3:15 pm

  35. TAHADHARI NA UMEME.

    1. Unazo nguvu umeme
    Niacheni niuseme
    Tafadhali usipime
    Kuuchezea umeme.

    2. Umeme ukiuseti
    Ndani tu ya kiberiti
    Huichanja mingi miti
    Bila kupita wakati.

    3. Milima wailipua
    Na hata kuipasua
    Umeme huitatua
    Mithili ya chandarua.

    4. Umeme nguvu unazo
    ‘Siufanyie mchezo
    Una akthari uwezo
    Wa kuzipa nguvu nyenzo.

    5. Unapoukalibia
    Umeme kuchungulia
    Usipotahadhalia
    Hatima utaumia.

    6.Umeme si lelemama
    Fikiri hilo daima
    Hii ni nasaha njema
    Mithili ile ya mama.
    ____________

    RWAKA RWA KAGARAMA
    MSHAIRI MNYARWANDA.

    Like

    Rwaka rwa Kagarama.

    March 16, 2016 at 5:32 pm

  36. Vipi mbona kimya mwanakwetu ???

    Like

    rwaka rwa kagarama

    February 12, 2017 at 9:39 pm


Leave a comment