simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Simba Mitaa ya Mjini / Lion in City Streets

leave a comment »

Ili tupate mazao bora hatuna budi kufuata kanuni bora za kilimo. Maendeleo ya teknolojia yameleta zana maalumu za kusaidia kuongeza tija katika kilimo. Ugunduzi wa pekee ulioleta mapinduzi ya kilimo katika mataifa yaliyoendelea ni pamoja na ule wa matrekta.

Picha ya kwanza inatuonyesha mazao ya migomba yalivyostawi vema na kumpa mkulima (Bw Vicent wa Morogoro) uwezekano wa kuongeza ubora wa maisha yake.

Picha ya pili – ni trekta la manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. Trekta hilo, kama yalivyo mengi kadhaa, linatumika kwa kazi ya kubeba taka kupeleka dampo. Ni kazi ya maana.

Ila, kwa maoni yangu, ijapokuwa kazi ya kuzoa taka ina umuhimu wake, mahali mwafaka kwa kulipeleka trekta ni shambani. Likalime. Likapalilie. Likapande. Likavune na kisha lisombelee mazao kupeleka ghalani. Taka zina zana zake maalumu. Kuna malori maalumu kwa ajili ya kazi ya kubeba taka. Malori hayo yameundwa vizuri kiasi kwamba yanapobeba taka – hutaona taka zikisambaa mitaani kwa kupeperushwa na upepo. Kumbe basi, trekta hili lipo MISPLACED. Ni sawasawa na kukuta Simba (mnyama mwitu) akikatiza mitaa ya katikati ya jiji. Si mahali pake. Ingawa naupongeza uongozi wa manispaa kwa kazi hiyo nzuri na ya maana, bado ninawashauri walete malori maalumu ya kusombea taka badala ya kutumia matrekta. Na matrekta hayo wayapeleke mashambani ili kuendelea Kilimo Kwanza. Ciao!

Una maoni gani?

Advertisements

Written by simbadeo

January 23, 2010 at 6:46 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: