simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Utajiri wa Watanzania

leave a comment »

Tanzania ni nchi iliyojaaliwa utajiri mwingi. Utajiri mkubwa zaidi ni ardhi. Pamoja na kuwa na utajiri huo bado Watanzania wengi ni maskini, kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za utafiti, hususan Poverty and Human Development reports (2002, 2003, 2005 na 2007). Wengi bado wanaishi kwa kipato cha chini ya dola 2.00 za Marekani kwa siku.

Kuna mengi ambayo serikali na Watanzania kwa ujumla tunaweza kufanya ili kujikomboa kutoka katika umaskini huu. Jambo kubwa ni kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa. Lingine ni kutoa nafasi kwa watu kueleza vipaumbele vyao katika maeneo yao na kuhakikisha kwamba wanashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi waliyoshiriki kuibuni.

Suala la ardhi na umiliki wake halina budi kuzingatiwa na kupewa uzito unaostahili. Tunayo Sheria ya Ardhi ambayo imechukua sura mbalimbali katika miaka tofauti. Umiliki wa ardhi mpaka sasa uko wa aina mbili. Kuna ule wa kimila na ule wa hati. Kwa kuwa umiliki wa aina zote hizo mbili unatambuliwa kwa mujibu wa sheria basi ni vema njia zote hizo zikapewa heshima iliyo sawa.

Upangaji wa matumizi ya ardhi ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa. Hata hivyo, ili kuepuka migogoro na manung’uniko ni vema wananchi wakapata fursa ya kuelewa vizuri mipango hiyo ya matumizi ya ardhi – pengine washiriki kikamilifu katika kuibuni na kisha wale ambao hawana budi kupisha miradi ya kitaifa na kieneo ya maendeleo, wapate kufanya hivyo kwa kuridhika baada ya kulipwa fidia inayostahili kwa kulinganisha na nguvu ya soko.

Ili basi nchi iendelee, kuna umuhimu mkubwa wa kuzingatia haki katika ushiriki wa watu kwenye mipango ya maendeleo, kusikiliza sauti zao na kuwaelimisha juu ya mipango iliyopo ili hata wanapolazimika kuhama kutoka eneo moja kwenda lingine wafanye hivyo kwa kuelewa umuhimu wa kuhama kwao.

Nakaribisha maoni kujadili jambo hili.

Advertisements

Written by simbadeo

January 6, 2010 at 5:01 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: