simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Road to Kisarawe…

leave a comment »

kisarawe22-4

Huu ndio mkeka wa kuelekea Kisarawe. Ni kiasi cha km 40 hivi kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam. Zamani safari ilichukua saa kadhaa, siku hizi ni safari ya dakika kadhaa tu. Ni mji mzuri kuutembelea. Umezungukwa na Msitu mnene wa Kazimzumbwi. Una madhari nzuri na ni eneo la juu ya milima. Kutoka Kisarawe unaweza kuona baadhi ya maeneo ya jiji la Dar, hasa yale yanayopakana na ufukwe wa Bahari ya Hindi.

Hali ya maisha haitofautiani sana na Dar.  Bei za bidhaa ni kama ilivyo pale Dar. Maji ndiyo tatizo kubwa kwa wakazi wa Kisarawe. Hata hivyo kuna juhudi kadhaa kujaribu kurekebisha hali hiyo.

kisarawe1-6

Ni moja ya jengo la zamani lililo upande wa mbele katika moja ya shule kongwe nchini Tanzania ya Minaki. Hapa kuna historia. Historia inayostahili kutunzwa. Kuna viongozi wengi wazito waliopata kusoma hapa. Naamini wakiamua wanaweza kubadili mwonekano wa mazingira ya shule hii maarufu na iliyo katika mandhari mazuri sana. Tukumbuke tulikotoka. (mtaniwia radhi kwa mkao wa picha, ni katika hekaheka za kupata picha kutoka kwenye gari lililo kwenye mwendo).

Advertisements

Written by simbadeo

December 30, 2008 at 9:11 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: