simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mjasiriamali kazini …

leave a comment »

 

 

Anaitwa Aboubakar. Mkazi wa jijini Dar. Ana takribani miezi miwili kwenye biashara hii. Hapo kabla alikuwa mfanyakazi (mhudumu) kwenye moja ya migahawa ya chakula katikati ya jiji. Ujira wake ulikuwa Sh. 2000 kwa siku (na free breakfast and lunch). Aliona maisha yanazidi kumbana.

Ameamua kujitosa kwenye biashara ya matunda. Anakodi mkokoteni kwa Sh. 500 kwa siku. Kwa bei ya sasa ya machungwa, kila moja analinunua kwa kati ya Sh. 40 na 50. Yeye analiuza kwa Sh. 100. Mzigo unaolala kwa siku ni kidogo. Amefaulu kupata kipato bora zaidi kutokana na kujiajiri kuliko alipokuwa ameajiriwa.

Tatizo kubwa analohofia ni mgambo wa jiji. Mgambo hawa huwakamata ‘wajasiriamali’ wa aina ya Aboubakar na kuwanyang’anya kila walicho nacho na kisha kuwatupa lupango. Aboubakar anauliza: “Hivi, kosa letu hasa ni nini? Je, wanataka tufanye kazi gani ili kujipatia riziki? Tukabe watu? Tupige debe kwenye vituo vya daladala?” Anashauri kuwa jiji lisiwahangaishe katika namna wanavyowahangaisha na kuwataabisha. Wawatengee maeneo maalumu kandokando ya barabara kuu. Wawatoze ushuru wa biashara na ushuru wa kufanya usafi maeneo hayo.

Ajira za uhakika katika viwanda, maduka makubwa, gereji n.k. bado ni kitendawili kwa vijana na wakazi wengi wa jiji hili. Kumbe, wale wanaojishughulisha katika shughuli hii na ile, wasaidiwe ili wafanye shughuli hizo kwa ufanisi zaidi. Ni kwa kuweka utaratibu mzuri kwamba vijana watajiajiri, watajipatia riziki, watalipa kodi serikalini na kwa kuwa watakuwa na shibe, basi hatutategemea kupata rabsha kutoka kwao. Kuna msemo wa Kiingereza unasema: A hungry man is an angry man. Tuwape shibe vijana ili wasiwe wenye hasira dhidi ya wengine (hasa dhidi ya watu wa tabaka la juu).

 

Advertisements

Written by simbadeo

June 19, 2008 at 6:15 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: