simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

‘Wachawi’ wapo kila mahali … siyo Bungeni peke yake

with one comment

Takribani kwa muda wa wiki moja hivi sasa, nchi yetu imetikiswa na imani za kishirikina. Chimbuko la mtikisiko huo likiwa ni katika mmoja wa mihimili mitatu inayolifanya dola letu, Bunge la Muungano. Kwa ufupi, ni jambo la kushangaza na kutia simanzi sana kuwa jambo hili limepewa uzito liliopewa. Hivi, unaamini katika uchawi wa kulogana? Unaamini kuwa mtu anaweza kukuwangia na kukuchawia na ukadhurika?

Nitasema imani yangu. Haya ni mambo ya imani. Kuna imani zenye msingi na ambazo ‘reasoning’ huzikubali. Kuna imani ambazo hata ‘a simple reasoning’ huzikataa. Kwa imani yangu, HAKUNA uchawi wa kulogana. Mimi nina tafsiri tofauti ya uchawi.

Tafsiri yangu ya uchawi na ambao tunaweza kuthibitisha kuwa unafanya kazi kweli ni hii: uchawi ni matendo yaliyo nyuma ya maumbo ya ulafi, kijicho, chuki, fitina, uzandiki, usengenyaji, ufisadi, uhujumu uchumi, kutowajibika, uvivu, uzembe, udanganyifu, ulaghai, kuendesha mambo kijanjajanja n.k. Mambo hayo yanajidhihisha katika maisha yetu ya kila siku. Matokeo yake mara zote ni mabaya kwa waathirika wa vitendo hivyo. Huo ndiyo uchawi, lakini si mambo ya kusema eti fulani anachukua udongo wa pale ulipokanyaga, anakwenda kuukaanga kwenye kigae na wewe uliye mbali kule unaanza kudhurika. Uchawi wa kulogana HAUPO.

Ndiyo sababu nilishangazwa kwa kiasi kikubwa na namna tukio la hivi karibuni kule Bungeni lilivyochukuliwa. Inaonyesha kuwa ni asilimia kubwa sana ya Watanzania ambao hawajavuka kizingiti cha ‘kuamini’ katika uchawi. What a shame!

Ukiiba. Wewe ni mchawi. Ukila rushwa. Wewe ni mchawi. Ukiingia mkataba kwa nia ya kujinufaisha wewe nakuwaangusha wengine, wewe ni mchawi. Ukimsingizia mwenzako mambo ya uongo katika sehemu yenu ya kazi na kisha mwenzako akafukuzwa kazi, basi wewe ni mchawi. Ukisengenya, wewe ni mchawi. Ukilaghai, wewe ni mchawi. Ukiibia mitihani, wewe ni mchawi. Ukionea wenzako kwa sababu ya madaraka au nafasi uliyo nayo, wewe ni mchawi. Ukiuza bidhaa zilizopitwa na muda wake wa matumizi, wewe ni mchawi. Kuna mambo mengi na matendo mengi tunayoweza kuyaweka katika kundi la uchawi.

Watanzania tubadilike. Tuwe serious na tufuatilie masuala yaliyo serious. Si ajabu kuna waheshimiwa Wabunge ambao badala ya kusoma kwa makini makabrasha ya bajeti ya 2008/2009 wao walibaki kushabikia mambo ya kishirikina, matokeo yake wanajiandaa kupitisha bajeti pasipo kuisoma kwa makini. Kumbe, bajeti yenyewe imejaa matundu kibao ambayo kwa kweli yanatia aibu wote waliohusika na mchakato wa maandalizi yake. Haiwezekani Wabunge wawili watatu tu ndiyo waone upungufu mkubwa uliojitokeza katika bajeti. Ipo haja ya kuwa serious zaidi na masuala yanayohusu maslahi na mustakabali wa Taifa kwa ujumla.

Nawakilisha.

 

Advertisements

Written by simbadeo

June 18, 2008 at 5:53 pm

Posted in Siasa na jamii

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. haipendezi kwa wabunge kuanza kupoteza utakatifu halizi wa bunge

    Like

    zephania lyamuya

    November 7, 2008 at 6:15 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: