simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Nyororo barabarani Dar …

leave a comment »

Ni magharibi. Jijini Dar. Nyororo linaloundwa na mto wa magari. Yanamiminika kuelekea pembezoni mwa jiji. Saa za asubuhi, mtiririko huwa ni kinyume chake. Mtiririko huelekea katikati ya jiji. Ndiyo mwendo wa maisha. Asubuhi mtiririko wa watu na magari kuelekea mjini. Jioni mtiririko wa watu na magari kuelekea pembezoni mwa jiji. Ni wimbo ambao mapigo yake ni yaleyale.

Je, kuna haja ya kubadili mapigo na midundo na mitiririko hii? Tubadili wimbo ili kwamba mtiririko usiwe wa mstari bali mtawanyiko. Mtawanyiko wenye uwiano. Uwiano utakaofanya mambo yaende sawa. Wimbo mpya. Nani awe mtunzi wa wimbo huu mpya? Bila shaka atapatikana kwa njia ya chaguzi. Chaguzi huru na za haki. Mimi na wewe tunaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kubadili wimbo huu. Tumechoka foleni. Foleni wakati wa kwenda mjini. Foleni wakati wa kwenda nyumbani. Foleni. Foleni.

Advertisements

Written by simbadeo

June 16, 2008 at 9:38 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: