simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Tuwape fursa…

with one comment

mchanganyikotanzania.jpg

staawakeshomiburanitemeke.jpg

watotompiranimiburanitemeke.jpg

Ni watoto kutoka Kata ya Miburani katika Manispaa ya Temeke katika Jiji la Dar es Salaam.

Tunaweza kusoma mengi katika picha hizi, baadhi yake ni:

1. Jamii yetu inaishi kwa kuchanganyika bila matatizo, hapa hakuna kuulizana kabila wala asili, sote tunaishi, tunacheza na kushirikiana katika mambo mbalimbali bila kujali tofauti zetu za dini, rangi wala utajiri. Kupoteza hali hii ni kazi ndogo. Hivyo, hatuna budi kuilinda kama tunavyolinda mboni za macho yetu.

2. Kuna vipaji miongoni mwa watoto na vijana wetu. Tuna jukumu la kubaini vipaji hivyo, kuviendeleza na kuvienzi ili viwaletee tija wale wanaohusika lakini pia kwa Taifa letu. Humu hatuna budi kusaka vipaji adimu vya kupeperusha vyema bendera ya Taifa letu.

3. Kuna matatizo ya viwanja vya michezo hapa nchini. Ujenzi holela unameza hata sehemu za wazi na viwanja vya michezo. Ipo haja ya kudhibiti hali hii. Kupanga miji yetu na kuzingatia kuweka maeneo ya wazi, ya bustani za kupumzikia, na viwanja vya michezo. Tuwe navyo vingi ili kuwaepusha wale wanaovitumia dhidi ya hatari mbalimbali kama vile tunavyoona katika picha kuwa magogo yako katikati ya kiwanja. Ni hatari na hali yenyewe ya kiwanja, kichanga kitupu, ni hatari pia.

Advertisements

Written by simbadeo

March 2, 2008 at 12:11 pm

Posted in Siasa na jamii

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. duh mpira wa miaka hiyo CHANDIMU mchangani.

    Like

    luihamu

    March 3, 2008 at 7:59 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: