simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Wajasiriamali…

with one comment

wajasiriamali.jpg

simbastreetphotosoctnov2007-276.jpg

Wanakusanya chupa tupu za kuhifadhia maji. Wanapopata kiasi kikubwa basi wanapeleka katika viwanda vinavyonunua kama malighafi ya kutengeneza bidhaa nyingine za plastiki.

Kwa hiyo wanasaidia kupunguza takataka kama hiyo iliyo kwenye picha ya chini katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar.

Pengine ni wakati sasa ufanyike uamuzi wa kuendesha operesheni kamambe ya kulisafifisha jiji dhidi ya taka za plastiki. Makampuni yanayozalisha bidhaa za aina hiyo ni wawe wadau wakubwa katika kampeni hiyo. Makampuni hayo yanafahamika. Kuna makampuni kama vile ya kuzalisha maji ya kunywa ya chupa, kuna makampuni ya kuzalisha mifuko ya plastiki ya kubebea bidhaa nyingine na kadhalika.

Makampuni haya yana jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa taka za plastiki zinadhibitiwa. Watenge bajeti maalumu kwa ajili ya kulipa watu watakaokuwa wanasomba taka hizo. Wawalipe vizuri ili hawa wahakikishe kuwa hakuna wanayoiacha nyuma. Makampuni haya haya yatenge bajeti maalumu kwa ajili ya kuelimisha wateja wao, kuwa mara wanapomaliza kutumia bidhaa zilizo katika chupa au mfuko wa plastiki basi wasitupe ovyo bali watupe katika maeneo maalumu yaliyowekwa kwa ajili hiyo katika sehemu mbalimbali za jiji.

Kwa hiyo, mwisho wa siku, tutakuwa na mji ulio safi (hata kama ni katika kiwango cha wastani), wapo watu ambao watapata ajira na polepole jamii itaanza kuelimika juu ya umuhimu wa kutunza mazingira na kuyaweka katika hali ya usafi.

Inawezekana. Kinachohitajika ni ‘will power’ ya wenye mamlaka.

Advertisements

Written by simbadeo

February 20, 2008 at 7:12 pm

Posted in Siasa na jamii

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. http://www.luihamu-rastafarian.blogspot has been deleted.
    Mkuu Simbadeo,sijui nianzie wapi lakini lazima nikugusi kwanini nimeamuwa kuachana na mambo ya blogu.Mkuu Simbadeo wewe ni kati ya watu ambao wamekuwa wakinipa saport ya kublog nami sina budi ya kukuaga.Kuna mambo mengi ambayo yamenifanya niache kublogu na moja kati ya hayo mambo ni maoni yangu kuto kukubaliwa na baadhi ya blogu.Comment ninazozitoa zinafutwa au kutojibiwa.Nakutakia kila la heri MkuuSimbadeo.JAH NUH DEAD,JAH RASTAFARIAN.

    Like

    luihamu

    February 22, 2008 at 12:00 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: