simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Bila shaka unajua hapa ni wapi … au siyo?

leave a comment »

Mlimani, Dar es Salaam University

Ni ndoto ya Watanzania wengi walio mashuleni. Ni mahali ambapo pamewezesha watu kubadili hali za kiuchumi za familia zao. Ni mahali ambapo pameacha alama njema za kudumu katika mioyo ya watu wengi. Wengi wamepita hapa. Wengi zaidi watapita hapa.

Tanzania, kama zilivyo nchi nyingi zinazoendelea, zinategemea sana vyuo vikuu katika vita dhidi ya umaskini. Ni miaka karibu 50 tangu Uhuru wa Tanganyika. Swali la kujiuliza hapa ni kwa kiasi gani Chuo hiki kikongwe nchini kimesaidia katika kupunguza umaskini wa Taifa la Watanganyika na Watanzania kwa ujumla wao. Je, Taifa liko katika mwelekeo sahihi wa kujikomboa dhidi ya umaskini na matatizo mengine kama maradhi na ujinga?

Tutafakari. Ikiwa wewe umewahi kupita hapa, je, umetumiaje elimu yako katika kupiga vita umaskini unaolikabili taifa letu? Au umetumia elimu yako kujinufaisha binafsi kwa njia za kifisadi? Je, tumewasaidiaje wengine nao wapate fursa ya kupita hapa? Je, kiwango cha ubora wa elimu kinachotolewa hapa kina nafuu zaidi leo kuliko kilivyokuwa hapa nyuma? Kama jibu ni hapana, nini kifanyike ili kuongeza ubora huo?

Yapo mengi ya kutafakari. Haya machache yanatosha kukuanzisha mlolongo wa tafakuri kuhusu maisha na maendeleo ya Watanzania.

Advertisements

Written by simbadeo

January 27, 2008 at 12:10 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: