simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Umeme …

with one comment

dscf0049.jpg

Kuanzia kesho (bado dakika 20 muda huu ninapoandika) umeme nchini Tanzania utapanda kwa asilimia 22. Ni ongezeko kubwa hasa katika kipindi hiki ambapo thamani ya shilingi imeshuka sana.

Pichani ni wateja waliofurika pale PATCO Supermarket, BP Dar es Salaam International Airport. Niliipiga saa 1.30 usiku, yaani kiasi cha saa 4.30 kabla ya kuingia mwaka mpya 2008. Wateja hawa wameamua kununua umeme leo kwa wingi kabla bei mpya kuanza rasmi hapo kesho tarehe 1 Januari 2008.

 Watu wanazidi kuwa ‘cost conscious’. Yule mlalahoi kama mimi anayenunua umeme wa shilingi 10,000 itampasa kuanza kulipa wastani wa shilingi 12,200 kwa umeme kiasi kilekile. Yeye akienda leo kununua umeme huo haokoi fedha nyingi. Lakini kibopa ambaye matumizi yake ni shilingi 100,000 basi kama alikuwepo kwenye msululu huo aliokoa shilingi 22,000. Unaweza kuona jinsi fedha inavyoanza kuwa kubwa.

Mungu ainusuru Tanzania. Umeme unavyopanda ndivyo bei za bidhaa nyingine nyingi zitakavyopanda. Sasa hivi tutasikia kuwa magazeti bei imepanda. Internet pia itakuwa gharama zaidi. Lo, Mungu tunusuru.

Advertisements

Written by simbadeo

December 31, 2007 at 11:49 pm

Posted in Uncategorized

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. Suluhushi si kununua umeme mwingi kabla bei haijapanda.Duh tutafika kweli?

    Like

    luihamu

    January 6, 2008 at 1:24 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: