simbadeo2000

Uhuru u wapi? (Where is Freedom?)

 Ni katika makutano ya barabara za Bibi Titi Mohammed na Uhuru. Chunguza vizuri. Kuna nguzo yenye kuelekeza barabara ya Uhuru. Chini ya nguzo hiyo kuna mtu amekaa. Amejishika tama. Kuza kidogo hiyo picha ili umwone vizuri.

Tunapata tafakari nzito. Ni miaka 47 tokea Uhuru. Hali ya uchumi wetu ikoje? Hali ya maisha ya watu wetu ikoje? Maisha yamekuwa magumu zaidi. Uhakika wa kesho unazidi kutoweka.  Uhuru tulio nao una maana gani? Hivi kwa nini tufike mahali ambapo watu wetu wengi wako kama huyu? Hawaishi kujishika tama? Kwa nini? Kwa nini watu wasukumwe na kuishia katika point ya kulipuka kama walivyolipuka kule Afrika ya Kusini? Niliwahi kuona lori limeandikwa ‘Sheria duniani, haki mbinguni’. Tutafakari. Tujadili. Tunakoenda siko. Azimio la Zanzibar limekuja na mengi. Haya ndiyo yanayozidi kututesa leo. Tumeweka kando ‘Ujamaa na Kujitegemea’. Tumebaki kuomba hata chakula wakati kila mahali katika Tanzania ukiweka mbegu au mche utaota na kukua. Sera. Siasa. Uongozi. Elimu. DUNI.

No Comments Yet »

Say something?Comments RSS TrackBack URI

About author

I am a citizen of Tanzania. I live in Dar es Salaam, commercial city of Tanzania. I am an editor, particularly dealing with books as well as other publications and related activities: editing, translating, supervising design and layout, monitoring printing, warehousing and dissemination of the books. I am also an author: I write children's story books, school textbooks and adult books. I undertake translation tasks from English to Kiswahili and vice versa. I do book indexing, that is preparing an index for a professional book. Contact: kakasimba@gmail.com . Feel free to get in touch with me.

Search

Navigation

Categories:

Links:

Archives:

Feeds