
Ni katika makutano ya barabara ya Nyerere na ile iendayo uwanja wa Ndege wa zamani, Terminal One. Kuanzia hapo, ni kimbembe kuikamata Banana. Barabara ni ya lane moja, lakini mara nyingine hujitokeza lanes mpaka tatu! Kuna wanaopita kwenye kingo za barabara, kuna wanaokatisha katika njia za waendao kwa miguu! Ni uharibifu mkubwa wa mazingira. Kuna umuhimu wa kutafuta suluhu kwa kadhia hii inayozidi kukua kila kunapokucha … foleni ndeeefu katika barabara za Dar es Salaam. Suluhu si kuondoa vipanya peke yake, kuna umuhimu wa wanausalama barabarani pia kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi. Foleni hizi ni jinamizi kubwa kwa kasi ya kukua kwa uchumi wetu. Dawa itafutwe.

Historia hii itunzwe. Ni hazina kubwa itakayolisaidia Taifa hili katika miaka ijayo. Hao wanaoitwa ‘waendelezaji’ waende kuendeleeza jiji huko pembezoni, siyo hapa katikati.
Na mvua inapotua jijini Dar mambo huwa hivi mitaani:

Mitaa hubaki mitupu.

Na baada ya mitaro ya maji machafu kuziba, basi maji hufurika barabarani. Hali hiyo inapotokea, unachagua moja kati ya mawili – au unajitosa kukanyaka maji hayo au kulipa sh 100 ili uvushwe katika maji machafu kwa kubebwa kwenye mkokoteni. Mababa wa Jiji, kazi mnayo!

Kikosi kamili cha Sitakishari Veteran Sports Club katika Bonanza Maalumu la kusherehekea kutimiza kwa mwaka mmoja tangu timu hiyo ianzishwe rasmi. Iliichapa timu ya Ukonga kwa mabao 2 – 0. Timu nyingine zilizoshiriki ni pamoja na Boko, Ukonga, Pugu, Kitunda na Air Wing. Kandanda safi ilisindikizwa na mchezo wa kuvuta kamba na burudani safi ya muziki.

Kulia ni Mh. Stambuli, Diwani wa Kata ya Kipawa aliyekuwa mgeni rasmi katika Bonanza hilo; kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Sitakishari Veterani Sports Club, Mr Morris; Kulia kwa Bwa Stambuli ni Mr Elly Ngwala, aliyekuwa DJ na mhamasishaji mkuu.

Mwanadada mshika kibendera alimudu vema mechi zote zipatazo nane alizosimamia tangu asubuhi.

Washikaji kibao walikuwepo.

Mambo ya kuvuta kamba hayakukosekana. Mpaka tunakwenda press, Bonanza lilikuwa bado likiendelea.

Ndiyo. Kiatu kimetulia. Na mguu kimepata. Ila Bongo yetu kwa kutotunza mazingira, kiboko. Hebu cheki hiyo chupa hapo pembeni.

Kijani ni afya. Utembeapo eneo lenye mimea kwa wingi tena inayotunzwa vizuri, unajisikia kuwa na hali tofauti katika akili, mwili na hata roho yako. Kijani ni afya.
Imefika wakati tusambaze ukijani kama huu mahali mbalimbali katika jiji hili. Mazingira ya namna hii yatachangia katika kuongeza ubora wa afya zetu. Tunapokuwa na afya njema, tuna nafsi ya kufiriki vizuri zaidi na kwa hiyo kujiletea maendeleo sisi wenyewe na taifa letu. Tushikamane kutunza mazingira ili mazingira yatutunze na kutuletea tija.
Picha inaonyesha eneo lililo karibu na makutano ya Barabara za Ohio, Bibi Titi na Ali Hassan Mwinyi.

Hii ni kuwatakia ‘A Happy Valentine’s Day’. Pichani mdau wa blog hii, Anna, wa Njia Panda Segerea, Dar es Salaam.

Kituo cha Basi cha Banda la Ngozi, Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam. Ni saa 11.10 jioni.
Imagine. Ulikuwa na siku ngumu. Siku ambapo ulitumia akili na nguvu nyingi katika kazi zako. Inapofika saa ya kutoka kazini, kituoni magari ya abiria yanakupita tu yakiwa yamejaa. Pengine ni wakati sasa tutafute ufumbuzi wa kudumu kuhusu usafiri wa umma ili mtu asisubiri zaidi ya dakika tano kituoni.

Ni Abdallah. Mwenyeji wa Mtwara. Anasema kazi yake hii inalipa zaidi kuliko kupalilia mikorosho kule Mtwara. Hapa jamii nzima ina wajibu. Nini kiwe vipaumbele vya Taifa letu: kuchuuza mali zilizotengenezwa na wenzetu wa nje au kutilia mkazo uzalishaji unaoliletea Taifa hili fedha za kigeni? Je, kwa nini kwa mfano isifike mahali Bw Abdallah akaona kuwa inalipa zaidi sana kupalilia korosho kuliko kuchuuza soksi (cheap) za kutoka Uchina? CCM ilyo madarakani ina kazi ya kuwaeleza wananchi mkakati wake wa kubadili kitendaguro hiki.

Ni gari namba T 489 ARN.

Ni eneo la Njiapanda Segerea, Barabara ya Nyerere. Wakaazi wakishangaa lori lililoyumba na kufanya kreti za za kinywaji kumwagika na kulamba vumbi. Bahati nzuri hakuna liyethubutu kunywa au kufanya uhalifu mwingine, mfano, kujaribu kuproa vinywaji vilivyosalimika. Ila kama kawaida, hakuna dogo mjini. Watu kibao. Ipo haja ya kutoendekeza sana kudodosadodosa baadhi ya mambo yanapotokea. Wapo waliouliza, je, ingekuwa petroli, watu bado wangebaki hapo huku kumbukumbu za matukio kama ya kule Mbeya na la hivi karibuni kule Nakuru Kenya ambapo lori la mafuta lilipata ajali na watu kujaribu kujichotea mafuta hayo? Watu wapatao 130 waliteketea kwa moto na wengine wengi kujeruhiwa.

Mlimani City, Dar es Salaam. Ingefaa kuwa na maeneo ya namna hii sehemu nyingi za Dar es Salaam na mikoani. Mahali pa kununua na kuuza. Wawekezaji wapewe uendeshaji wa masoko yetu hata yale tunayoita ‘Soko Mjinga’. Hii haimaanishi kuwa ‘wawekezaji lazima wawe wa kutoka nje. Watanzania wenzetu wanaweza kuendesha sehemu kama hizi na kuweka viwango bora vya ubora.

Mlimani City in the making. Ni eneo la kupendeza. Kama si kubananisha sana nyumba, ingefaa nyumba nyingi mitaani zijengwe kwa muundo huo – hasa katika high density areas – kwani makazi bora ni muhimu kwa maendeleo ya kiakili, kiafya, kiroho na kwa aina zote za ukuaji. Inafaa kutembelea hapa.