Picha hii imepigwa jana saa 12.15 jioni pale ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Huenda mimi nimepitwa na wakati. Nilipokuwa kwenye mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria nilijifunza kuwa Bendera ya Taifa hushushwa kutoka kwenye mlingoti kila ifikapo saa 12 kamili jioni.
Inawezekana ni mimi ndiye niliyepitwa na wakati au inawezekana kabisa wale wenye jukumu la kushusha bendera hii pale ofisini kwa Mzee Kandoro walipitiwa wakati saa za mwishomwisho za 2007 zikiyoyoma.
Inawezekana pia ni ishara kuwa Watanzania huwa hatujali muda. Tunapanga wenyewe lakini ni sisi sisi ndiyo tunaovunja ahadi za muda tulizoweka. Wakati ni mali. Nidhamu katika kutunza muda ni muhimu kwa maendeleo ya aina yoyote ile.
Nawatakia HERI na MAFANIKIO katika mwaka huu mpya wa 2008 ambao sasa hivi una umri wa nusu saa hivi.
Kila la kheri.