Congo Street … kizaazaa
Mtaa wa Congo, kama nilivyoukuta jana. Hekaheka kama zamani … kupita ni lazima iwe ubavuubavu …
Tranforma katika makutano ya Mtaa wa Congo na Aggrey lilileta mtafaruku wakati nikipita pale, majira ya saa sita mchana. Kuna shoti ilitokea na kuunguza baadhi ya nyaya. Jambo hilo lilizua mtafaruku mkubwa. Katika umati huo … ilikuwa vigumu watu kujiokoa.
Wapo walioibiwa … wapo walioiba …
Ndivyo inavyoonekana. Kwa mujibu wa wafanyabiashara katika eneo hilo, tukio hilo la kulipuka halikuwa mara ya kwanza. Imetokea mara nyingi. Inafaa Tanesco wafanyie kazi jambo hili kabla matatizo makubwa hayajatokea. Tafadhali badilisheni transforma hiyo. Yawezekana muda wake umekwishapita na haifai tena kuendelea kutoa huduma.






