Usafirishaji … biashara kubwa
Transport. Usafirishaji inazidi kuwa biashara kubwa nchini Tanzania. Kadiri shughuli za kiuchimi zinavyokua ndivyo sekta hiyo nayo inavyozidi kushamiri. Usafirishaji uko katika ngazi zote. Kuanzia mizigo yenye uzito mdogo kwa kutumia vyombo vidogovidogo vya usafirishaji hadi biashara kubwa. Kwa vile sisi ni nchi yenye bahari, kuna fursa kubwa sana za kuifanya biashara hii itoa mchango mkubwa zaidi katika uchumi wa nchi ikiwa ni pamoja na kutoa ajira nyingi zaidi kwa vijana wetu. Itazamwe kwa makini na kuwekewa mipango madhubuti ili kusukuma mbele taifa letu.



