
Ni katika makutano ya barabara ya Nyerere na ile iendayo uwanja wa Ndege wa zamani, Terminal One. Kuanzia hapo, ni kimbembe kuikamata Banana. Barabara ni ya lane moja, lakini mara nyingine hujitokeza lanes mpaka tatu! Kuna wanaopita kwenye kingo za barabara, kuna wanaokatisha katika njia za waendao kwa miguu! Ni uharibifu mkubwa wa mazingira. Kuna umuhimu wa kutafuta suluhu kwa kadhia hii inayozidi kukua kila kunapokucha … foleni ndeeefu katika barabara za Dar es Salaam. Suluhu si kuondoa vipanya peke yake, kuna umuhimu wa wanausalama barabarani pia kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi. Foleni hizi ni jinamizi kubwa kwa kasi ya kukua kwa uchumi wetu. Dawa itafutwe.